Pata taarifa kuu

DRC: Ujumbe wa mratibu wa mazungumzo ya amani kuzuru Goma

NAIROBI – Ujumbe kutoka Ofisi ya mratibu wa mazungumzo ya amani Mashariki mwa DRC kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, unatarajiwa kuzuru Goma, kuthathmini maendeleo ya hali ya usalama.

Aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Aliyekuwa rais wa Kenya Uhuru Kenyatta © Monicah Mwangi / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Haijawa wazi iwapo Kenyatta naye atakuwa miongoni mwa wajumbe hao, ambao kazi yao itakuwa ni kuandaa ripoti itakayowasilishwa kwa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, wanaotarajiwa kukutana baadae mwezi huu, kujadili hali ya usalama Mashariki mwa DRC.

Wajumbe hao watathatmini mafanikio na changamoto za kikosi cha Jumuiya ya Afrika Mashariki ambacho kilitumwa mwaka uliopita, kusaidia kuleta amani na kuwaondoa waasi wa M 23 katika maeneo ambayo walikuwa wanadhibiti.

Ziara hii inakuja katika kipindi ambacho kikosi hicho kimepata Kamanda mpya Meja Jenerali Alphaxard Kiugu kutoka Kenya, baada ya kuondoka kwa mtangulizi wake Meja Jenerali Jeff Nyagah.

Haya yanajiri siku chache baada ya rais Felix Thisekedi, kunukuliwa akisema hajafuraishwa na utendakazi wa kikosi cha Jumuiya kuhusu nama kinavyokabiliana na waasi wa M 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.