Pata taarifa kuu

Idadi ya waliofariki katika mafuriko na maporomoko ya udongo nchini Rwanda yafikia 130

NAIROBI – Nchini Rwanda, baadhi ya watu zaidi ya 130 waliopoteza maisha kufuatia mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo, wameanza kuzikwa katika mikoa ya magharibi,kusini na kaskazini mwa  nchi hiyo.

Mafuriko na maporomoko ya udongo yasababisha hasara kubwa nchini Rwanda, zaidi ya watu 100 wakiwa wamefariki
Mafuriko na maporomoko ya udongo yasababisha hasara kubwa nchini Rwanda, zaidi ya watu 100 wakiwa wamefariki REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu Edouard Ngirente ameongoza mazishi ya baadhi ya watu hao huko Rubavu, Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, huku rais Paul Kagame akisema, maafisa wa serikali wamefanya walichoweza kuwaokoa watu waliothiriwa na mafuriko hayo.

Katika hatua nyingine, naibu msemaji wa serikaliAlain Mukuralinda,amesema maeneo ya  Rubavu, Karongi, Rutsiro, Nyabihu  na  Ngororero ndiyo yaliyoathirika zaidi.

Aidha amedokeza kuwa zaidi ya nyumba elfu tano zimesombwa na maji ya mafuriko, mengi yazo zikiwe katika wilaya ya Rubavu, huku nyumba zingine 2 500 zikiwa zimeachwa kwenye hali mbovu.

Miundo mbinu kama vile mabomba ya maji, mitambo ya mawasiliano na umeme imetajwa pîa kuharibiwa.

Juhudi za pamoja kati ya wizara mbali mbali zimewekwa kusaidia kwenye shughuli ya uokoaji, wakiwemo maofisa wa kutoka ofisi ya waziri mkuu.

Mbali na Rwanda, mvua kubwa inayonyesha, imesababisha maafa na madhara makubwa katika nchi jirani za Uganda, Kenya na Tanzania.

Watalaam wa hali ya hewa wanatabiri kuwa mvua kubwa itaendelea kunyesha nchini Rwanda mwezi huu wa tano.

Haya yanajiri wakati huu pia serikali ya Rwanda ikisema kuwa juhudi za kuwatafuta watu waliopotea na pia kuwaokoa walio hai zinaendelea baada ya kutokea mafuriko makubwa na maporomoko ya udongo, Magharibi na Kaskazini mwa nchi hiyo ambapo watu mia moja ishirini na saba kupoteza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.