Pata taarifa kuu

Museveni: Maofisa wafisadi watapata adhabu kukiwemo kufungwa jela

NAIROBI – Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema maafisa wa serikali watakaopatikana kuhusika na ufisadi, watachukuliwa hatua kali ikiwemo kufungwa jela.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. via REUTERS - PRESIDENTIAL PRESS SERVICE
Matangazo ya kibiashara

Museveni ametoa kauli hiyo baada ya kukamatwa na kuzuiwa kwa mawaziri watatu, wanaodaiwa kuiba mabati yaliyopaswa kuwajengea makaazi watu masikini kutoka eneo la Karamoja.

Moja ya tatizo letu kubwa ni ufisadi, unaofanywa na watumishi wa serikali na hili linarudisha nyuma ukuaji wetu, amesema Museveni wakati akihudhuria maadhimisho ya miaka sita ya Kumbukumbu ya Joan Kagezi iliyofanyika huko Munyonyo.

Mwezi Machi, rais aliagiza idara ya upelelezi DDP na polisi kuanzisha uchunguzi kuhusu madai ya utumizi mbaya wa mabati, yaliyolenga kuifaidi jamii katika eneo la Karamoja.

Tangu kipindi hicho, mawaziri watatu wamemakatwa akiwemo Mary Goreti Kitutu, Amos Lugolobi, wawili hawa wako nje kwa dhamana, wakati huu Agnes Nandutu akiendelea kuzuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mahakama siku ya Alhamisi, Aprili 27, ilimzuilia Joshua Abaho, kwa tuhuma sawia na hizo za utumizi mbaya wa mamlaka.

Wanasiasa wa upinzani wameendelea kuishtumu serikali ya rais Museveni kutochukua hatua kali dhidi ya watu wanaojihusisha na ufisadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.