Pata taarifa kuu

DRC : CENI yaongeza muda wa zoezi la uandikishaji wapiga kura

NAIROBI – Nchini DRC, tume ya uchaguzi nchini humo, CENI imeongeza muda wa siku 10 wa zoezi la uandikishaji wapiga kura kwenye baadhi ya maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo, kutoa nafasi kwa watu zaidi kujitokeza kushiriki.

Tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI imeongezeka muda wa kuwasijili wapiga kura kwenye baadhi ya maeneo ya mashariki
Tume ya uchaguzi nchini DRC, CENI imeongezeka muda wa kuwasijili wapiga kura kwenye baadhi ya maeneo ya mashariki © John Wessels - AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukuliwa sambamba na kuwasili kwa wanajeshi wa Burundi, Sudan Kusini na Uganda jimboni Kivu Kaskazini, ambapo wanaunda sehelu ya kikosi cha wanajeshi wa jumuia ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo, maswali bado yapo kuhusu iwapo kuwasili kwa vikosi hivyo kunatosha kuhakikisha shughuli hiyo inaendelea bila changamoto ya kiusalama na hata kuruhusu shughuli hiyo kuanza katika maeneo yanayodhibitriwa na M23.

Hadi kufikia sasa, usajili wa wapiga kura katika maeneo yanayoshikiliwa na waasi wa M23 bado haujaanza, vifaa vya usjaili havijapelekwa na wala tarehe ya shughuli hiyo kuanza haijatangazwa.

Juma lililopita wanaharakati kadhaa pamoja na wanasiasa walitoa mwito kwa tume ya uchaguzi nchini humo CENI, kuongeza muda wa usajili wa wapiga kura katika maeneo ambayo hali ya usalama imerejea, ili kutoa nafasi kwa raia wengi zaidi kujiandikisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.