Pata taarifa kuu

Mtoto wa rais wa Uganda aahidi kutuma wanajeshi kuilinda Moscow

Mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, Muhoozi Kainerugaba, amesema atatuma wanajeshi wa Uganda kuilinda Moscow iwapo kutatokea tishio la "mabeberu".

Muhoozi Kainerugaba, kulia, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, huko Entebbe, Uganda, Mei 7, 2022.
Muhoozi Kainerugaba, kulia, mtoto wa Rais wa Uganda Yoweri Museveni, huko Entebbe, Uganda, Mei 7, 2022. AP - Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

"Mniite 'mshirika wa Putin' mkitaka, sisi Uganda tunapaswa kutuma wanajeshi kuilinda Moscow ikiwa itatishiwa na mabeberu," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter. "Nchi za Magharibi zinapoteza muda wao kwa propaganda zisizo na maana za kuiunga mkono Ukraine," ameongeza mtoto wa kiume wa rais Kaguta Museveni, mfuasi mkubwa wa Vladimir Putin.

Pia alitangaza siku ya Alhamisi kuundwa kwa kituo cha televisheni na redio yenye chapa yake, "MK". Bw. Kainerugaba, 48, anayezoea kutoa kauli tata kwenye Twitter, mwezi huu alitangaza kuwania kiti cha urais mwaka 2026.

Mnamo Oktoba 18, 2022, Yoweri Museveni alisema kwamba mwanawe wa pekee - ambaye pia ana watoto watatu wa kike - hatatweet tena kuhusu masuala ya nchi, baada ya mfululizo wa jumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter zenye utata mapema mwezi Oktoba ambapo alitishia kuivamia Kenya.

Uganda imejizuia katika kura za Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Ukraine, ikiwa ni pamoja na moja ya mwezi Februari katika kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, ambayo iliitaka Moscow kuondoa wanajeshi wake nchini humo. Mnamo mwezi Julai, wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov barani Afrika, Bw Kainerugaba alisema, akimaanisha Urusi: "Tunawezaje kuwa dhidi ya mtu ambaye hajawahi kutudhuru".

Urusi tangu jadi imekuwa na uhusiano mkubwa na Afrika kutokana na uungaji wake mkono kwa vuguvugu la kudai uhuru katika bara hilo. Waangalizi wamekuwa wakifikiria kwa muda mrefu kuwa Muhoozi Kainerugaba alipendekezwa kuchukua wadhifa huo kutoka kwa babake Yoweri Museveni mwenye umri wa miaka 78.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.