Pata taarifa kuu

DRC: Abiria 10 wauawa baada ya mashua yao kushambuliwa

NAIROBI – Nchini DRC, watu 10 wameuawa wiki hii baada ya kushambuliwa na watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami kwa silaha kwenye mashua iliyokuwa na abiria 200 Wilayani Kwamouth, wakiwa safarini kuelekea mjini Mbandaka.

Watu wenye silaha wameshambulia raia waliokuwa kwenye boti wakielekea Mbandaka
Watu wenye silaha wameshambulia raia waliokuwa kwenye boti wakielekea Mbandaka Junior D. KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Majambazi waliokuwa na silaha walishambulia mashua hiyo ilipokuwa imesimama katika kijiji cha Kaba l'école. kijiji Kilichoko  kati ya Kongo Brazzaville na Kwamouth ambako kiongozi wa kijiji hicho alikuwa miongoni mwa waathiriwa waliouawa. Pius Makina ni kiongozi wa eneo la Kwamouth.

“Kwa mujibu wa mtu akiyekuwa ndani ya mashua hiyo, abiria zaidi ya 200 walikuwa katika Mashua hiyo ambapo ni 22 tu wameonekana wengine hawajulikani waliko na zaidi ya watu 100 walizama na miili 9 imepatikana.”ameelezaPius Makina ni kiongozi wa eneo la Kwamouth.

00:20

Pius Makina ni kiongozi wa eneo la Kwamouth

Watu wenye silaha wamekuwa wakifanya mashambulio kwenye kingo za Mto Kongo. Guy Musomo ni mbunge wa Kwamouth

Ni makundi ambayo hayajulikani ila kuna walinda usalama ambao inabidi wafanye kazi.” ameeleza Guy Musomo ni mbunge wa Kwamouth.

00:20

Guy Musomo ni mbunge wa Kwamouth

 

Sababu ya shambulio hilo bado haijajulikana lakini eneo la Kwamouth limekuwa likikabiliwa na ukosefu wa usalama tangu mwezi Juni mwaka jana kufuatia mzozo kati ya jamii mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.