Pata taarifa kuu

Uganda: Wanaume sita wakamatwa kwa kujihusisha na 'mapenzi ya jinsia moja'

Wanaume sita wamekamatwa nchini Uganda kwa kujihusisha na 'mapenzi yajinsia moja', msemaji wa polisi ameliambia shirika la habari la AFP siku ya Ijumaa, siku moja baada ya Rais Yoweri Museveni kutangaza watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja kuwa "wamepotoka".

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni © StateHouseUganda
Matangazo ya kibiashara

"Kupitia mtandao wa kijasusi, tuliwakamata wanaume hao sita kwa kufanya mapenzi ya jinsia moja katika chumba kimoja huko Jinja", mji ulio umbali wa kilomita 80 mashariki mwa mji mkuu wa Kampala, amesema James Mubi, msemaji wa polisi.

"Tumearifiwa kuwa wote sita ni sehemu ya kundi kubwa la Jinja linalojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na tunatoa wito kwa umma kutoa taarifa kwa polisi zitakazowezesha kukamatwa kwa wanachama wengine wa kundi hilo," ameongeza.

Katika taarifa Alhamisi, mkuu huyo wa nchi mwenye umri wa miaka 78, ambaye ametawala nchi hiyo tangu 1986, alisema: "Mashoga wanapotoka sheria." Aliongeza kuwa "Nchi za Magharibi zinapaswa kuacha kupoteza wakati kwa ubinadamu kwa kujaribu kulazimisha mazoea yao kwa wengine."

Wabunge katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki ambako mapenzi ya jinsia moja ni kinyume cha sheria wanajiandaa kupitisha mswada, ambao ulipelekwa kwenye kamati ya bunge mapema mwezi Machi, ambao unatoa adhabu kali kwa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Nakala hii, ambayo inaamsha upinzani wa mashirika ya kutetea haki za binadamu, inatoa hadi miaka kumi jela kwa mtu yeyote anayejihusisha na vitendo vya ushoga au anayedai kuwa katika jamii ya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (LGBT +). Inatarajiwa kujadiliwa bungeni wiki ijayo, na kura ikiwezekana mapema siku ya Jumanne.

Mnamo 2014, Mahakam ya Uganda ilizuia mswada ulioidhinishwa na wabunge na kutiwa saini na Rais Museveni wa kuadhibu uhusiano wa jinsia moja na kifungo cha maisha. Nakal hii ilizua hasira nje ya mipaka ya Uganda, baadhi ya nchi tajiri zikiwa zilisitisha misaada yao baada ya kuwasilishwa Bungeni.kwa jukumu lake katika uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Ukraine tangu uvamizi wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.