Pata taarifa kuu

DRC: Fayulu amshutumu raisTshisekedi kuhusu utovu wa usalama mashariki mwa nchi

NAIROBI – Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Martin Fayulu, mmoja wa viongozi wakuu wa upinzani wa nchi hiyo, amemshutumu rais Félix Tshisekedi kuhusika moja kwa moja katika mvutano kamili na viongozi wa Rwanda wanaotuhumiwa kuwaunga mkono waasi wa M23  mashariki mwa DRC.

Martin Fayulu, Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC
Martin Fayulu, Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC © RFI
Matangazo ya kibiashara

Aidha, anaishtumu serikali kwa kupanga kile tunachoshuhudiwa.

“Ni vigumu sana mtu aje kusaidia taifa ambalo limekataa kutangaza vita dhidi ya mvamizi wake, inayokataa kufunga mipaka yake na mvamizi huyo na kusitisha uhusiano wa kidiplomasia.”ameeleza Martin Fayulu.

Haya yanajiri wakati huu baadhi ya wabunge wa DRC kutoka eneo linaloshuhudia machafuko jimboni Kivu Kaskazini, sasa wanamtaka rais Felix Tshisekedi, kufikiria upya uwezekano wa kuwa na mazungumzo na waasi wa M23.

Wabunge hao kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa nchini DR Congo wamedai kughadhabishwa na vita vinavyo endelea kati ya jeshi la Congo na waasi wa M23 ,nakuomba utatuzi haraka wa kisiasa.

Uongozi wa DRC umeendelea kuituhumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 madai ambayo Kigali imeendelea kukana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.