Pata taarifa kuu

Kigali: 'Mauaji ya Kishishe' ni 'uzushi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo'

Serikali ya Rwanda imejibu katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu shutuma za nchi hiyo kuunga mkono kundi la waasi la M23 mashariki mwa DRC. Msaada, ambao kila mara unakanushwa na Kigali, kwa mara ya kwanza uliolaaniwa na Ufaransa siku ya Jumatatu.

Watu walionusurika katika mkasa wa Kishishe ni nadra kutaka kutoa ushahidi, huku wakazi wakiendelea kufika miji mingine, kama hapa Kanyaruchinya, karibu na mji wa Goma, Desemba 5, 2022.
Watu walionusurika katika mkasa wa Kishishe ni nadra kutaka kutoa ushahidi, huku wakazi wakiendelea kufika miji mingine, kama hapa Kanyaruchinya, karibu na mji wa Goma, Desemba 5, 2022. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, mamlaka za Rwanda imezungumzia mauaji ya Kishishe mwishoni mwa mwezi Novemba, yaliyohusishwa waasi wa  M23 na Umoja wa Mataifa, ambapo watu 131 waliouawa kwa mujibu wa uchunguzi wa awali. 

Kwa mujibu wa serikali ya Kigali, "mauaji ya Kishishe" ni "uzushi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo", ambao ulisambazwa bila kufanyiwa uchunguzi wowote na shirika linaloaminika". 

Siku mbili baada ya shutuma za kwanza dhidi ya Rwanda, zilizoletwa na Ufaransa, na matamko ya makansela kadhaa wa Magharibi, kuitaka nchi hiyo kusitisha uungaji mkono wowote kwa M23 mashariki mwa DRC, serikali inakanusha, kwa mara nyingine tena, kuwa na uhusiano wowote na waasi. Kigali inasema Kuishutumu Rwanda kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 la Kongo ni uongo, na kunageuza sababu halisi za mzozo huo na matokeo yake kwa usalama wa nchi jirani. 

 Badala yake taarifa hiyo imesema  jumuiya ya kimataifa inapaswa kuwa na wasiwasi kuhusu "mateso" ya jamii za watu wanaozungumza Kinyarwanda  na Watutsi wa Kongo, ambao kulingana nao wanakabiliwa na matamshi ya chuki yaliyoidhinishwa na serikali ya DRC. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.