Pata taarifa kuu

Shule zafungwa katika kusaidia kupambana dhidi ya maambukizi ya virusi vya Ebola

Nchini Uganda, Shule zimefungwa kuanzia leo, kusaidia katika mapambano dhidi ya maambukizi ya Ebola, licha ya Wizara ya afya kusema, maambukizi yameanza kushuka.

Aidha, WHO imetanagza itatuma aina tatu za chanjo kwa ajii ya majaribio, ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo vya Ebola ambavyo havina chanjo iliyothibitishwa.
Aidha, WHO imetanagza itatuma aina tatu za chanjo kwa ajii ya majaribio, ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo vya Ebola ambavyo havina chanjo iliyothibitishwa. AFP - BADRU KATUMBA
Matangazo ya kibiashara

Agizo la kufungwa mapema kwa shule zote nchini humo, lilitolewa mapema mwezi huu baada ya wanafunzi wanane, kupatikana na maambukizi ya Ebola. 

Hatua hii pia inakuha, wakati huu Waziri wa afya Jane Ruth Aceng akisema kuwa, maambukizi yameanza kupungua katika jiji la Kampala,na Wilaya zilizoathiriwa zaidi za Mubende na  Kassanda . 

Waziri huyo amesema wananchi wameanza kufahamu kuwa maambukizi haya ni hatari na yanaua na wamezidisha umakini, suala ambalo amesema limesaidia kuzuia maambukizi zaidi. 

Shirika la afya duniani mimesema kufikia tarehe 22 mwezi huu, hakuna maambukizi yaliyowahi kurpotiwa kwa siku tisa zilizopita jijini Kampala, siku 10 huko Mubende na 12 katika Wilaya ya Kassanda. 

Aidha, WHO imetanagza itatuma aina tatu za chanjo kwa ajii ya majaribio, ili kuzuia maambukizi ya virusi hivyo vya Ebola ambavyo havina chanjo iliyothibitishwa.  

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.