Pata taarifa kuu

Uganda: 11 wafariki katika ajali ya moto shule ya wasioona

Takriban watu 11, wengi wao wakiwa watoto, wamefariki dunia na sita kujeruhiwa katika kisa moto kilichotokea katika shule ya walemavu wa macho huko Luga, kijiji kilicho kilomita 45 mashariki mwa mji mkuu wa Uganda Kampala, polisi imesema leo Jumanne.

Kisa hiki cha moto kilizuka huko Luga, kijiji kilicho kilomita 45 mashariki mwa mji mkuu wa Uganda Kampala.
Kisa hiki cha moto kilizuka huko Luga, kijiji kilicho kilomita 45 mashariki mwa mji mkuu wa Uganda Kampala. REUTERS - ABUBAKER LUBOWA
Matangazo ya kibiashara

Chanzo cha moto huo, uliozuka majira ya saa saba usiku Jumanne, saa za Afrika ya Mashariki, "hivi sasa hakijulikani lakini kwa sasa vifo kumi na moja (...) vimethibitishwa na watu sita walio katika hali mbaya wamelazwa katika hospitali ya Herona huko Kisoga", mji mkubwa  jirani, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

"Wengi wa waliofariki ni watoto," Jenerali Kahinda Otafiire, Waziri wa Mambo ya Ndani ameliambia shirika la habari la AFP.

“Rambirambi zetu ziendee kwa familia za marehemu (...), tutachunguza sababu za moto huo na iwapo kuna wahalifu watakamatwa”, ameongeza.

Shule ya Vipofu ya Salama, iliyojengwa mwaka wa 1999, inapokea wanafunzi kadhaa, wenye umri wa miaka 6 hadi 25.

"Sina maneno ya kuelezea uchungu ninaopitia," Richard Muhimba, baba wa mtoto aliyefariki ambaye anaishi katika mji wa karibu wa Mukono, ameliambia shirika la habari la AFP.

“Nilimtembelea Jumamosi, alikuwa na afya njema, na siku tatu baadaye anafariki,” amesema kwenye simu kabla ya kukata simu huku akiingiwa na huzuni.

Katika miaka ya hivi karibuni, visa kadhaa vya moto shuleni vimesababisha vifo vingi katika nchi hii ya Maziwa Makuu.

Mnamo mwezi wa Novemba 2018, watoto kumi na mmoja wamlifariki baada ya kisa cha moto kuzuka katika mabweni yao kusini mwa nchi. Mnamo mwezi wa Aprili 2008, wasichana 18 wa shule walifariki dunia, pia baada ya kisa cha moto kuzuka katika bweni lao, katika eneo la kilomita thelathini kutoka mji mkuu.

Mnamo mwezi wa Machi 2006, watoto wasiopungua 13 waliuawa na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati moto ulipozuka katika shule ya Kiislamu magharibi mwa Uganda. Mnamo mwezi wa Julai mwaka huo huo, watoto sita walifariki baada ya kisa cha moto kuzuka mashariki mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.