Pata taarifa kuu

Kesi za kwanza za Ebola katika jimbo la Kampala

Uganda imerekodi wagonjwa 14 wa Ebola katika jimbo kubwa la Kampala, waziri wa afya ametangaza siku ya Jumatatu, wakati akitaka kuwahakikishia wakaazi wa mji mkuu kwamba hali imedhibitiwa.

Kulingana na WHO, Uganda imerekodi tangu mwanzoni mwa 2020 takriban wagonjwa169,200 wa Uviko, na vifo 3,630.
Kulingana na WHO, Uganda imerekodi tangu mwanzoni mwa 2020 takriban wagonjwa169,200 wa Uviko, na vifo 3,630. © AP/Hajarah Nalwadda
Matangazo ya kibiashara

"Inazidi kutisha kwani visa vimerekodiwa Kampala," amesema Rebecca Nanyonga, mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 27.

Ugonjwa wa Ebola ambao umekuwa ukiendelea katika nchi hii ya Maziwa Makuu tangu mwishoni mwa mwezi Septemba umeua watu 44, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza Oktoba 19.

Mamlaka ya afya ya Uganda ilisema siku ya Jumatatu kwamba nchi hiyo imerekodi wagonjwa 90, vikiwemo vifo 28. Takwimu zilizochapishwa na mamlaka ya Kampala zinahesabu vifo kati ya wagonjwa waliothibitishwa.

Waziri wa Afya Ruth Jane Aceng ameliambia shirika la habari la AFP kwamba kumekuwa na kesi 14 zilizothibitishwa katika jimbo la Kampala pekee katika siku mbili zilizopita, ambapo 9 ni kesi za watu waliotangamana na mtu aliyefariki huko Kassanda, moja ya wilaya mbili katikati mwa nchi, kitovu cha janga hilo.

"Ugonjwa uko kati yetu"

Lakini wakaazi wa mji mkuu, wenye wakazi wapatao milioni 1.5, wanaendelea kuwa na wasiwasi. "Serikali imefanya kidogo kuwaelimisha wakazi wa Kampala kuhusu virusi vya Ebola," Bi. Nayonga amesema, huku akiongeza: "sherehe na matamasha bado yanaendelea. , lakini ugonjwa upo miongoni mwetu".

Maambukizi ya binadamu ni kupitia maji maji ya mwili, dalili kuu zikiwa ni homa, kutapika, kutokwa na damu na kuhara. Magonjwa ya mlipuko ni vigumu kudhibiti, hasa katika maeneo ya mijini.

Uganda imekumbwa na milipuko kadhaa ya Ebola, ambayo mara ya mwisho ilikuwa mwaka wa 2019. Kwa sasa hakuna chanjo dhidi ya aina ya virusi vya Ebola, vinavyojulikana kama "Strain ya Sudan", ambayo kwa sasa inaendelea nchini humo.

WHO ilitangaza mnamo Oktoba 12 kwamba majaribio ya kliniki ya chanjo dhidi ya aina hii yanaweza kuanza "katika wiki zijazo" nchini Uganda.

"Nilipumzika wakati kesi za Covid zilipungua, lakini sasa ninarudisha vizuizi, pamoja na kutembelea nyumbani kwangu," Ronald Kibwika, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 45, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana na WHO, Uganda imerekodi tangu mwanzoni mwa 2020 takriban wagonjwa169,200 wa Uviko, na vifo 3,630.

"Tuko kwenye rehema za Mungu ikiwa kesi za Ebola zitaongezeka Kampala, kwa sababu watu wengi hawachukui tahadhari za afya, na huduma za afya ni duni," amesema Anita Kwikiriza, mfanyabiashara mwenye umri wa miaka 31.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni aliamuru mnamo Oktoba 15 kufungwa kwa wilaya za Kassanda na Mubende, vitovu vya janga la ugonjwa huo, kwa marufuku ya kusafiri, amri ya kutotoka nje na kufungwa kwa maeneo ya wazi kwa umma.

Lakini Waziri wa Afya alitaka kutia moyo Jumatatu, akisema kuwa hali ya Kampala "imedhibitiwa na kwamba hakuna haja ya kuzuia shughuli za watu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.