Pata taarifa kuu

Watu wengine saba waambukizwa virusi vya Ebola Uganda

Wizara ya afya nchini Uganda, imethibitisha kuambukizwa kwa watu wengine saba, ugonjwa wa Ebola, baada ya mlipuko kuripotiwa wiki hii katika eneo ma Mubende, Magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha kifo cha mwanamume mwenye umri wa miaka 24. 

Vituo vya afya huko Bwera, karibu na mpaka wa DRC nchini Uganda, Juni 14, 2019.
Vituo vya afya huko Bwera, karibu na mpaka wa DRC nchini Uganda, Juni 14, 2019. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa afya wanasema aina hii ya virusi, ni Ebola Sudan iliyogunduliwa mwaka 2012. 

Kituo cha kudhibiti magonjwa barani Afrika, CDC kinasema Uganda imejiandaa vema kupambana na mlipuko huo, kulingana na Daktari, Ahmed Ogwell Ouma  Mkurugenzi Mkuu wa CDC. 

Mataifa jirani kama Kenya na Tanzania, yametangaza umakini katika mipaka yake na Uganda, kuhakikisha kuwa virusi hivyo havisambai. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.