Pata taarifa kuu

Moderna kuanzisha kiwanda chake cha kwanza cha chanjo barani Afrika nchini Kenya

Kampuni ya kutengeneza chanjo kutoka Marekani, Moderna, imetangaza Jumatatu wiki hii ujenzi wa kiwanda chake cha kwanza cha chanjo barani Afrika nchini Kenya, baada ya kutia saini makubaliano ya awali na nchi hii ambayo hutoa uzalishaji wa dozi milioni 500 kwa mwaka.

Kampuni ya Moderna inakusudia kuwekeza dola milioni 500 (euro milioni 460) katika kiwanda hiki, ambacho kitatoa chanjo ya messenger RNA kwa bara zima la Afrika, ambalo bado halina dozi za kupambana na Covid-19.
Kampuni ya Moderna inakusudia kuwekeza dola milioni 500 (euro milioni 460) katika kiwanda hiki, ambacho kitatoa chanjo ya messenger RNA kwa bara zima la Afrika, ambalo bado halina dozi za kupambana na Covid-19. AP - Joseph Odelyn
Matangazo ya kibiashara

Kampuni hiyo inakusudia kuwekeza dola milioni 500 (euro milioni 460) katika kiwanda hiki, ambacho kitatoa chanjo ya messenger RNA kwa bara zima la Afrika, ambalo bado halina dozi za kupambana na Covid-19.

"Mapambano dhidi ya janga la Covid-19 katika miaka miwili iliyopita yamekuwa ukumbusho wa kazi inayohitajika ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa huduma ya afya. Moderna imedhamiria kuwa sehemu ya suluhisho," amesema Stephane Bancel, mkurugenzi wake mkuu, katika taarifa kwa vyombo vya habari.

Moderna inasema inatumai kuwa kiwanda hiki kitaanza kusambaza chanjo yake ya Covid-19 barani Afrika mwaka ujao, kwa nia ya kuongeza chanjo katika nchi ambazo hazina kinga dhidi ya virusi hivyo.

"Uwekezaji wa Moderna nchini Kenya utasaidia kuelekea katika upatikanaji sawa wa chanjo duniani kote na ni ishara ya maendeleo ya kimuundo ambayo yatawezesha Afrika kuwa injini ya ukuaji endelevu wa kimataifa," Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema.

Zaidi ya mwaka mmoja baada ya dozi ya kwanza duniani ya chanjo ya Covid kutolewa, ni 12.7% tu ya watu bilioni 1.3 barani Afrika wamechanjwa kikamilifu.

Janga hili limedhihirisha utegemezi mkubwa wa bara hilo kwa chanjo zinazoagizwa kutoka nje.

Mwaka jana, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuundwa kwa kitovu cha chanjo nchini Afrika Kusini, kwa lengo hasa la kutoa uhamisho wa teknolojia kwa nchi nyingine, ikiwa ni pamoja na Kenya.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, raia wa Ethiopia, ametoa wito mara kwa mara wa upatikanaji sawa wa chanjo ili kukomesha janga hili na amekosoa nchi tajiri kwa kunyima dozi za kupambana na Covid-19.

Kwa sasa, ni 1% tu ya chanjo zinazotumiwa barani Afrika zinazozalishwa barani humo.

Nchi za Kiafrika, pamoja na nchi zingine zinazoendelea, zinatoa wito kwa Shirika la Biashara Ulimwenguni kuondoa hati miliki za chanjo na matibabu dhidi ya Covid, ili kuwezesha uzalishaji wa  dawa za mseto.

Ulaya ilipinga ombi hilo, ikisema kipaumbele ni kujenga uwezo wa uzalishaji katika nchi maskini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.