Pata taarifa kuu

EU yarejesha misaada kwa Burundi, mashirika ya kiraia, wanasiasa wakosoa

Umoja wa Ulaya, juma hili umetangaza kuwa utaanza kuipatia misaada ya kifedha nchi ya Burundi, ikiwa ni hatua zilizochukuliwa sambamba na Marekani mwaka uliopita, uamuzi ambao umekashifiwa vikali na wakosoaji wa Serikali ya Bujumbura.

Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye nchi yake imeondolewa vikwazo na Umoja wa Ulaya
Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye, ambaye nchi yake imeondolewa vikwazo na Umoja wa Ulaya TCHANDROU NITANGA AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, umoja wa Ulaya umesema umechukua hatua hii kutokana na hatua muhimu zilizopigwa na Serikali ya Bujumbura kuelekea demokrasia ya kweli baada ya uchaguzi wa mwezi Mei mwaka 2020.

Β 

Umoja wa Ulaya ukidai nchi hiyo imefungua ukurasa mpya wa amani ambo umeibua tumaini jipya kwa raia.

Β 

Mwaka 2016, EU ambayo wakati huo ndio ilikuwa mfadhili mkubwa wa Serikali ya Burundi, ilisitisha misaada yake kwa nchi hiyo kwa kile ilichodai kukithiri kwa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu na kushindwa kuzua machafuko y amara baada ya uchaguzi wa mwaka 2015.

Β 

Tangu kuingia madarakani kwa rais Evariste Ndayishime, baada ya kifo cha mtangulizi Wake Pierre Nkurunziza, umoja wa Ulaya ulionesha nia ya kuiondolea vikwazo nchi hiyo.

Β 

Licha ya kuwa katika taarifa yake umoja wa Ulaya umesema bado taifa hilo linakabiliwa na changamoto ya ulinzi wa haki za binadamu, utawala bora, maridhiano na utawala wa sheria, imeona inafaa kuondoa vikwazo zaidi kuruhusu hatua kupigwa.

Β 

Hata hivyo mashirika ya kiraia pamoja na wanasiasa wa upinzani nchini Burundi, Β wamekashifu hatua hii waliyosema ni usaliti kwa raia, wakiutuhumu umoja wa Ulaya na Marekani kupuuza ripoti ya hivi karibuni ya umoja wa Mataifa, iliyodai umlinzi wa haki za bindamu kwenye taifa hilo umezorota tangu kuingia madarakani kwa rais Ndayishimiye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.