Pata taarifa kuu
TANZANIA-COVID 19

Watanzania wahimizwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Covid 19

Nchini Tanzania, licha ya Wizara ya afya kuwataka raia kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya COVID 19, imebainika kuwa hatua idadi kubwa ya watu hawachukui tahadhari hizo hasa uvaaji wa barakoa wakiwa sehemu yenye mikusanyiko.

Raia wengi Tanzania hawazingatii mashari ya kudhibiti Corona.
Raia wengi Tanzania hawazingatii mashari ya kudhibiti Corona. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Rais Samia Suluhu Hassan akiwa ziarani mkoani Morogoro, ameendelea kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuchukua tahadhari wakati huu akitangaza ongezeko la wagonjwa wa corona katika miji mbalimbali.

Ripoti zinaeleza kuwa hospitali Kuu ya Bugando Wilayani Mwanza, imeripoti kushuhudia uhaba wa gesi aina ya oxygen, wakati huu wagonjwa wakiendelea kuongezeka.

Mkuu wa Hospitali hiyo Fabian Masaga, amesema kuna ongezeko la wagonjwa wanaotumia hewa hiyo muhilu na juhudi zinfanyika, kupata mitungi zaidi.

Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa rais Samia aliyeingia madarakani mwezi Machi, amebadilisha namna nchi hiyo inavyopambana na janga hilo kwa kuhimiza wananchi kuchukua tahadhari na nchi hiyo sasa imejiunga na mfumo wa Kimataifa wa Covax, ili kupokea chanjo kwa ajili ya watu wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.