Pata taarifa kuu
KENYA

Kenya kukabiliana na ongezeko la visa vya magonjwa ya akili

Kenya imezindua mpango kazi wa miaka mitano kukabiliana na ongezeko la visa vya magonjwa ya akili tangu nchi hiyo ilipoanza kukabiliwa na janga la Covid 19 mwezi Machi mwaka uliopita.

Takwimu za Wizara ya afya nchini zinaeleza kuwa asilimia 11 ya Wakenya wanasumbuliwa na magonjwa ya akili, sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wanaokwenda hospitalini kupata huduma za afya.
Takwimu za Wizara ya afya nchini zinaeleza kuwa asilimia 11 ya Wakenya wanasumbuliwa na magonjwa ya akili, sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wanaokwenda hospitalini kupata huduma za afya. TONY KARUMBA AFP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu za shirika la afya duniani zinaonesha kuwa ongezeko la visa vya magonjwa ya akili nchini Kenya vinaongezeka kwa sababu watu wengi wamepotea ajira na hata kupelekea kuwepo kwa visa vya watu kujitoa uhai hasa vijana wenye kati ya umri 15 na 29.

Kukabiliana na changamoto hii, Wizara ya afya nchini humo imesema itatenga fedha na kutoa elimu kwa wahudumu wa afya pamoja na kufungua vituo zaidi vya kuwapa tiba wagonjwa wa akili.

Takwimu za Wizara ya afya nchini zinaeleza kuwa  asilimia 11 ya Wakenya wanasumbuliwa na magonjwa ya akili, sawa na asilimia 25 ya wagonjwa wanaokwenda hospitalini kupata huduma za afya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.