Pata taarifa kuu

Dunia yaukaribisha mwaka mpya wa 2024

Nairobi – Dunia imeikaribisha mpya wa mwaka 2024 kwa furaha, kwa maombi na fataki.

Watu walifurika katika Makanisa, kulbi za starehe na maeneo mengine kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024
Watu walifurika katika Makanisa, kulbi za starehe na maeneo mengine kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024 AP - Yuki Iwamura
Matangazo ya kibiashara

Jiji la Sydney na Auckland yalikuwa maene ya kwanza kuukaribisha mwaka mpya.

Watu walifurika katika Makanisa, klabu za starehe na maeneo mengine kuuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024.

Sherehe za mwaka mpya nchini Australia
Sherehe za mwaka mpya nchini Australia via REUTERS - STRINGER

Hali imekuwa hivyo kwa wananchi wa nchi za Afrika Mashariki, huku viongozi wa nchi mbalimbali wakiwahotubia raia wao na kueleza mipango ya mwaka mpya.

Samia Suluhu Hassan ni rais wa Tanzania.

‘‘Mwaka 2024, tutaadhimisha miaka 60 ya muungano na miaka 60 ya mapinduzi matukufu ya Zanzibar.’’ alieleza rais Samia.

00:14

Rais Samia Hassana

Nchini Kenya, rais William Ruto alikuwa katika Ikulu ndogo ya Nakuru.

Sherehe za mwaka mpya jijini Paris
Sherehe za mwaka mpya jijini Paris AP - Aurelien Morissard

Aliwahotubia Wakenye ambao mwaka 2023 wamelalamikia ugumu wa maisha. Ruto amekuwa na ujumbe huu kwa wanaopinga sera za serikali yake.

‘‘Tutahakikisha kuwa uhuru wa taasisi zetu hauzui watu kuchukuliwa hatua na kuwajibika, lazima tuwe makini ili tusitumie katiba vibaya kwa kuwatesa wanachi walio wengi.’’ alisema rais Ruto.

00:25

Rais William Ruto

Naye rais wa Rwanda Paul Kagame, ametumia hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2023 kukanusha madai ya nchi jirani za Burundi na DRC kuwa, Kigali inayumbisha usalama wao.

‘‘Dunia ya sasa tumezoea kuambiwa kuwa watu wana masilahi, hakuna suala la uthibitisho wala ushahidi, hawajali kama ni kweli au hapana, Rwanda tumewahi kuwa peke yetu, hatuongopi kuwa huenda siku moja tukabaki peke yetu.’’ alisema rais Kagame.

00:22

Rais Paul Kagame

Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron amesema mwaka huu wa 2024 utakuwa wa kujivunia kwa taifa lake, kwa sababu, nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa Michezo ya Olimpiki na kufunguliwa kwa Kanisa la Notre-Dame.

Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron amesema mwaka huu wa 2024 utakuwa wa kujivunia kwa taifa lake
Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron amesema mwaka huu wa 2024 utakuwa wa kujivunia kwa taifa lake © AFP / PEDRO PRADO
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.