Pata taarifa kuu

COP28: Makubaliano ya rasimu ya kumaliza utumizi wa mafuta ya kisukuku

Rasimu ya hivi punde iliyotolewa na umoja wa mataifa, kuhusu hali ya hewa duniani imeainisha njia zote za muhimu kuchukua, kuanzia kumaliza matumizi ya mafuta ya Visikuku hadi kutojadili kabisa njia hizo.

Wanaharakati waandamana dhidi ya mafuta ya kisukuku katika Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa COP28, Jumanne, Desemba 5, 2023, huko Dubai, Falme za Kiarabu.
Wanaharakati waandamana dhidi ya mafuta ya kisukuku katika Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa COP28, Jumanne, Desemba 5, 2023, huko Dubai, Falme za Kiarabu. AP - Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Hatma ya mafuta, gesi na makaa ya mawe ni miongoni mwa masuala mtambuka yanayojadiliwa kwenye mkutano huo, ambapo nchi zimegawanyika kuhusu hatua za kuchukua kumaliza matumizi yake.

Katika rasimu hii, kuna mapendekezo matatu yanayojadiliwa na ambayo ni wazi huenda nchi zisifikie makubaliano, ikiwemo suala la uwepo wa mkataba wa kisheria kuzilazimisha nchi kuachana na matumizi ya mafuta ya visikuku.

Mapendekezo ya awali yalikuwa na vipengele viwili peke yake, ikiwemo kuachana kabisa na matumizi ya nishati hiyo au kuchukua hatua za kupunguza.

Mjadala kuhusu matumizi ya mafuta ya visikukuu, umeshuhudia kwa mara ya kwanza uwepo wa idadi kubwa ya wajumbe wanaojaribu kuzishawishi nchi wazalishaji wa mafuta kutoachana kabisa na nishati hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.