Pata taarifa kuu

Mkutano wa kujadili kuundwa kwa mkataba wa kisheria kuhusu uchafuzi wa plasitiki unafanyika Nairobi

Nairobi – Wajumbe kutokana mataifa mbalimbali wanakutana jijini Nairobi kwa Kikao cha tatu cha kamati ya kimataifa kinachojadili mchakato kuelekea kuundwa kwa mkataba wa kisheria wa kimataifa, kuhusu uchafuzi wa plasitiki.

UNEP
Nchi wanachama za umoja wa mataifa zinatarajiwa kuafikiana kuhusu mkataba huu kufikia 2024 REUTERS - JOHN GEDDIE
Matangazo ya kibiashara

Nchi wanachama za umoja wa mataifa zinatarajiwa kuafikiana kuhusu mkataba huu kufikia 2024.

Kikao hiki kinafuatia vikao vingine viwili vilivyofanyika mwishoni mwa mwaka jana nchini Uruguay na mwezi mei mwaka huu jijini Paris Ufaransa.

Mkurugenzi wa shirika la umoja wa mataifa linalohusika na mazingira UNEP, Inger Andersen, amesema mkataba huu unatakiwa kuimarisha mabadiliko ya kimfumo ikiwemo kama vile, mifumo ya kupunguza, kutumia tena na kuichakata.

‘‘Ni lazima mkataba huu wa kisheria uondoe matumizi yasio ya lazima ya bidhaa zinazotumika mara moja, na kuangazia ugeukiaji wa bidhaa zisizo za plastiki, plasitiki mbadala, na bidhaa mbadala ambazo hazileti madhara makubwa.’’ alisema Inger Andersen.

00:14

Inger Andersen- Mkurungenzi wa UNEP

Kwa upande wake rais wa Kenya, William Ruto, amesema takwimu za uchafuzi wa plastiki zinaashiria haja ya dunia kufanya kazi pamoja.

‘‘Tishio la plastiki kwenye sayari yetu, afya yetu na mustakabali wetu wa baadaye ni lenye uzito sana na linatuhitaji sisi sote, na namaanisha sisi sote, kuja na mkataba wa kimataifa na kuhakikisha utekelezaji wake utakaotusaidia kupambana na tishio la plastiki kwenye dunia yetu.’’ aliezleza rais William Ruto.

00:19

William Ruto- Rais wa Kenya

Kulingana na UNEP, kila mwaka, takriban tani milioni 400 za taka za plastiki huzalishwa duniani, huku kati ya tani milioni 8 na 10 ya taka hizi zikiishia kwenye mazingira ya baharini kila mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.