Pata taarifa kuu

Uzalishaji wa mafuta ya kisukuku unarejesha nyuma juhudi za kuelekea matumizi ya nishati safi

Kinyume na ahadi za kupunguza uzalishaji wa mafuta, sera za serikali duniani kote zitaongeza maradufu uzalishaji wa nishati hiyo katika mwaka 2030, ripoti mpya kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira (UNEP) ilifichua hapo jana.

Inger Anderson- Mkuu wa UNEP
Inger Anderson- Mkuu wa UNEP AP - Nariman El-Mofty
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi mkuu wa UNEP, Inger Anderson, amesema mipango ya serikali kuongeza uzalishaji wa mafuta ya kisukuku inarejesha nyuma juhudi za kuelekea kwenye matumizi ya nishati safi na kuhatarisha mustakabali dunia.

Inger hata hivyo amesema kuwezesha chumi za mataifa na nishati safi ni nji apekee kumaliza umasikini wa nishati pamoja na kupunguza utoaji wa gesi chafu.

Kwa upande wake katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, amesema kuwa dunia haiwezi kuangazia janga la tabianchi bila ya kukabiliana na chanzo kikuu, utegemezi wa mafuta ya kisukuku.

Mkuu wa UN amesema dunia haiwezi kuangazia janga la tabianchi bila ya kukabiliana na chanzo kikuu, utegemezi wa mafuta ya kisukuku
Mkuu wa UN amesema dunia haiwezi kuangazia janga la tabianchi bila ya kukabiliana na chanzo kikuu, utegemezi wa mafuta ya kisukuku © Craig Ruttle / AP

Aidha amesema kwamba dunia inahitaji ahadi za kuaminika ili kuzidisha matumizi ya nishati jadidifu, kuondoa matumizi ya mafuta ya kisukuku na kuongeza ufanisi nishati. 

Ripoti hii aidha imebainisha kuwa nchi zilizo na uwezo mkubwa kuondokana na matumizi ya mafuta ya kisukuku zinatakiwa kuongeza malengo yao ya upunguzaji pamoja na kusaidia michakato ya kuondokana na mafauta hiyo katika nchi zenye rasilimali ndogo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.