Pata taarifa kuu

Uhamiaji, matokeo ya 'uporaji' wa Afrika, ashutumu rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Idadi kubwa ya wahamiaji wa Kiafrika kuelekea Ulaya ni matokeo ya "uporaji" na "ubeberu wa nchi za Magharibi" barani Afrika, rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin Archange Touadéra ameshtumiwa siku ya Alhamisi mbele ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, kwenye Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, Septemba 21, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Faustin-Archange Touadera, kwenye Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa, Septemba 21, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ulimwengu mzima umefuata kwa masikitiko makubwa kuwasili kwa maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika kwenye kisiwa cha Lampedusa nchini Italia katika siku za hivi karibuni," ametangaza kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa huko New York, akielezea vijana wa Kiafrika ambao "wanatafuta sana kuingia katika nchi za bara la Ulaya kutafuta maisha".

"Kuongezeka huku kwa mzozo wa wahamiaji ni moja ya matokeo ya kutisha ya uporaji wa maliasili za nchi, zilizofanywa maskini na utumwa, ukoloni na ubeberu wa nchi za Magharibi, ugaidi na migogoro ya ndani ya kivita, ambayo mara nyingi hufunguliwa kwa malengo ya ku maslahi binafsi, mivutano ya siasa za kijiografiambinu za kimkakati  kati ya mataifa makubwa yenye nguvu duniani,” ameshutumu.

Maoni haya yanasikika kama jibu kwa yale ya Jumatano jioni ya Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni ambaye alithibitisha katika jukwaa kwamba Afrika "sio bara maskini", lakini "tajiri wa rasilimali za kimkakati".

Kisiwa cha Italia cha Lampedusa, kilicho chini ya kilomita 150 kutoka pwani ya Tunisia, kinawakilisha mojawapo ya vituo vya kwanza vya wahamiaji wanaovuka bahari ya Mediterania wanaotarajia kufika Ulaya.

Kati ya Jumatatu na Jumatano wiki iliyopita, karibu watu 8,500, zaidi ya wakazi wote wa Lampedusa, waliwasili kwa boti 199, kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji.

Wahamiaji hawa hasa wanatoka Afrika, kupitia Tunisia.

Rais Touadéra amesifu "mshikamano na juhudi za ajabu zinazofanywa na nchi zinazowahifadhi" na Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi kuwapokea wahamiaji hawa.

Pia ameshutumu "wasafirishaji haramu na wauzaji wa binadamu" na kutoa wito kwa Umoja wa Mataifa kushirikisha nchi za Afrika "katika kutafuta suluhu za kimataifa za migogoro ya uhamiaji na changamoto zilizopo zinazowakabili vijana wa bara hilo."

Siku ya Jumatano, Giorgia Meloni, akizungumzia kumiminika kwa wingi kwa wahamiaji huko Lampedusa, alitoa wito kwa Umoja wa Mataifa "kutogeuzia macho yake mbali na janga hili" na "kuanzisha vita visivyo na huruma dhidi ya wafanyabiashara haramu wa binadamu".

Lakini "Afrika si bara maskini. Kinyume chake, ina rasilimali nyingi za kimkakati," alisema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.