Pata taarifa kuu

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wafunguliwa katikati ya mizozo

'Wiki ya ngazi ya juu' ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa unafunguliwa huko New York siku ya Jumanne. Mkutano utakaohudhuriwa na viongozi wa dunia na ambao Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa wito wa kuuweka chini ya ishara ya hatua. Katika ajenda ya mkutano huo ni pamoja na kurejea kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs), yaliyopitishwa mwaka 2015 na Umoja wa Mataifa.

Makao makuu ya Umoja wa Mataifa kabla ya Mkutano Mkuu wa wiki hii huko New York, Jumapili Septemba 17, 2023.
Makao makuu ya Umoja wa Mataifa kabla ya Mkutano Mkuu wa wiki hii huko New York, Jumapili Septemba 17, 2023. AP - Bryan Woolston
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia Jumatatu hii asubuhi, wakuu wa nchi na serikali 145 wanatarajiwa New York kwa wiki ya "ngazi ya juu" ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambayo inaanza tena kwa kasi kamili kwa mara ya kwanza tangu janga la Uviko. Ajenda hiyo inatoa nafasi kwa mada zinazodaiwa na nchi zinazoendelea, huku kukiwa na mikutano ya ana kwa ana inayotarajiwa na matumaini ya kusonga mbele na machafuko ya Haiti na Sudan, na ikiwezekana kuanzishwa tena kwa mazungumzo katika Mashariki ya Kati. Na bila shaka vita nchini Ukraine.

Pia katika ajenda ya mkutao huu ni pamoja na kuzinduliwa upya kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yaliyopitishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa mwaka 2015 ili kujenga mustakabali bora na endelevu zaidi ifikapo mwaka 2030. Wakati watu walio katika mazingira magumu zaidi wameathiriwa sana na maporomoko ya machafuko, nusu tu 15% ya SDGs hizi ziko vizuri, nyingi zinadumaa na zingine zinarudi nyuma.

'Mpango wa usalama'

Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu yaliwekwa kwa matumaini ya ajabu mwaka 2015. Yanadaiwa kusaidia kumaliza umaskini uliokithiri duniani ifikapo mwaka 2030 kwa kushughulikia sababu zake kama vile njaa, ukosefu wa elimu au maji au hata uchafuzi wa mazingira. Hakuna cha kufurahiya. Mnamo mwaka wa 2023, umaskini uliokithiri uliongezeka kwa mara ya kwanza katika miaka thelathini, migogoro mingi, ikiwa ni pamoja na matokeo ya kimataifa ya vita vya Ukraine na kabla ya hapo mgogoro wa afya ambao ulionyesha kutokuwepo kwa mshikamano wa kimataifa, umefanya malengo ya maendeleo endelevu kutofikiwa, kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.