Pata taarifa kuu

BRICS inalenga kuongeza nchi wanachama, kutoka 5 za sasa

Nairobi – Wakati huu mkutano wa wakuu wa nchi za muungano wa BRICKS wakitarajiwa kukutana hapo kesho nchini Afrika Kusini, moja ya ajenda kubwa itakayowekwa mezani ni kuhusu kuongeza nchi wanachama, kutoka 5 za sasa.

Miongoni mwa nchi za hivi karibuni kuonesha nia ya kujiunga na muungano huo ni pamoja na Iran na Argentina
Miongoni mwa nchi za hivi karibuni kuonesha nia ya kujiunga na muungano huo ni pamoja na Iran na Argentina © Radio Algérienne
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa nchi za hivi karibuni kuonesha nia ya kujiunga na muungano huo ni pamoja na Iran na Argentina, wakiwa na dhumuni moja tu la kuweka usawa wa kidunia kushindana na mataifa mengine ya magharibi.

Wakati huu ambapo muungano huo unaonesha kutoridhishwa na hali ya sasa ya mfumo wa kidunia, nchi za BRICKS ambazo ni pamoja na Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini, zimeahidi kuufanya muungano wao kuwa wenye ushawishi duniani licha ya kushindikana kwa miradi yake kadhaa.

Nchi ya Afrika Kusini ambayo ndio mwenyeji wa kongamano hili la 15, imesema zaidi ya mataifa 40 yameonesha nia ya kujiunga na muungano wao, huku karibu nusu yake zikiandika baraua rasmi ikiwemo DRC.

Hata hivyo licha ya kuwa karibu asilimia 40 ya raia walioko kwenye muungano huo wanachangia robo ya pato ghafi la dunia, lengo la kuwa jumuiya yenye ushawishi kiuchumi na kisiasa halijaweza kufikiwa kutoka na mgawanyiko na kutofautiana katika masuala muhimu ya kidunia.

Rais wa Urusi pekee Vladimir Putin, ndie hatohudhuria mkutano huu kutokana na hati ya kimataifa ya kukamatwa kwakwe iliyotolewa na mahakama ya ICC, ambapo Afrika Kusini ni mtekelezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.