Pata taarifa kuu

Wakafanyikazi 62 wa misaada wameuawa kote duniani: UN

Nairobi – Jumla ya wafanyakazi wa misaada 62 wamepoteza maisha mwaka huu duniani kote, imesema taarifa ya umoja wa Mataifa, wakati huu UN ikijiandaa kufanya kumbukizi ya miaka 20 tangu kutekelezwa kwa shambulio baya zaidi kwenye makao makuu yake mjini Baghdad.

Kwa mujibu wa UN, nchi ya Sudan Kusini kwa miaka kadhaa imeendelea kuwa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa misaada
Kwa mujibu wa UN, nchi ya Sudan Kusini kwa miaka kadhaa imeendelea kuwa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa misaada REUTERS - BRENDAN MCDERMID
Matangazo ya kibiashara

Kila tarehe 19 ya mwezi Agost, Umoja wa Mataifa huadhimisha siku ya kimataifa ya kibinadamu, kukumbuka shambulio la bomu la kujitoa muhanga ambalo liligharimu maisha ya watu 22, akiwemo aliyekuwa mkuu wa tume ya UN nchini Iraq, Sergio Vierra de Mello.

Mbali na wafanyakazi 62 kuuawa ndani yam waka huu katika maeneo yenye mizozo, wengine 84 walijeruhiwa na 34 kutekwa nyara, kwa mujibu wa taasisi ya ulinzi wa wafanyakazi wa misaada.

Kwa mujibu wa UN, nchi ya Sudan Kusini kwa miaka kadhaa imeendelea kuwa hatari zaidi kwa wafanyakazi wa misaada, ambapo mpaka kufikia mwezi huu kumeripotiwa mashambulio 40 na wafanyakazo wake 22 kuuawa.

Mataifa mengine yaliyotajwa kukithiri kwa mashambulio ya wafanyakazi wa misaada ni pamoja na Sudan, Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Mali, Somalia, Ukraine na Yemen.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.