Pata taarifa kuu

Kasi ya utoaji wa chanjo kwa watoto yaanza kuongezeka : UN

Nairobi – Umoja wa mataifa unasema, kasi ya utoaji chanjo kwa watoto imeanza kuongezeka baada ya kushuka kwa kiwango cha juu wakati wa janga la mlipuko wa Uviko19, hata hivyo wataalamu wakisema bado kuna upungufu.

Utoaji wa chanjo kwa watoto yaanza kuongezeka kwa mujibu wa WHO na UNICEF
Utoaji wa chanjo kwa watoto yaanza kuongezeka kwa mujibu wa WHO na UNICEF REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja ya WHO na UNICEF, watoto milioni 4 walipokea chanjo za awali mwaka uliopita, ukilinganisha na mwaka 2021.

Mkuu wa masuala ya chanjo kutoka shirika la afya duniani, Kate O’Brien, amesema hii ni habari njema na kwamba kwa wastani, mataifa mengi duniani yameanza kurejesha kinga mwili ambayo ilikuwa thabiti kabla ya mlipuko wa virusi vya Korona.

Kwa upande wake mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema anakubaliana na takwimu hizi mpya na licha ya kuonya kuwa lazima nchi ziongeze juhudi kuhakikisha zinawafikia watoto wengi kadiri inavyowezekana.

Hata hivyo pamoja na dunia kupiga hatua, watoto zaidi ya milioni 20 ama walikosoa chanjo ya Kwanza au ya pili mwaka 2022, ikiwa ni pungufu kutoka watoto milioni 24 mwaka uliotangulia, ambapo asilimia 84 ya watoto mwaka uliopita walipokea chanjo ya Surua.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.