Pata taarifa kuu

Zaidi ya watu bilioni tatu wanakabiliwa na baa la njaa duniani: FAO

Watu  zaidi ya  bilioni 3 duniani wanakabiliwa na baa la njaa kutokana na athari za janga la Uviko 19 ,vita vya Ukraine na mabadiliko ya tabia nchi, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa wiki hii na shirika la umoja wa mataifa la chakula na kililimo, FAO.

Shirika na WFP na USAID yamekuwa yakiwasaidia raia wanaokabiliwa na njaa nchini Kenya kupata chakula
Shirika na WFP na USAID yamekuwa yakiwasaidia raia wanaokabiliwa na njaa nchini Kenya kupata chakula Kabir Dhanji - WFP / Kabir Dhanji
Matangazo ya kibiashara

Katika ukanda wa Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki,watu zaidi ya milioni 15 ,milioni nane wakiwa na watoto ,wameathirika ,ukosefu wa usawa ukizidi kufanya hali hiyo kuwa mbaya.

David Abudho kutoka Shirika la kimsaada la Oxfam, nchini Kenya akizungumzia ripoti hiyo, amesema inasikitisha kuwa hali hiyo hujurudia kila mara kutokana na uwekezaji mdogo unaowekwa kwenye mikakati ya msaada na kumaliza ukosefu wa usawa.

Afisa huyo kutoka shirika la Oxfam, alizungumza na mwandishi wetu Carol Korir kuhusu hali hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.