Pata taarifa kuu

Kongamano la mataifa kuhusu ufadhili wa miradi ya kulinda mazingira latamatika Paris

Nairobi – Mkutano wa kimataifa unaolenga kufanya mabadiliko katika mfumo wa kimataifa wa kifedha, unatarajiwa kutamatika hivi leo jijini Paris, baada ya hapo jana hatua kadhaa kupigwa katika kuondoa mzigo wa madeni kwa nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na mzozo wa kiuchumi na athari za tabianchi.

Kongamano la mataifa kuhusu ufadhili wa miradi ya kulinda mazingira latamatika Paris
Kongamano la mataifa kuhusu ufadhili wa miradi ya kulinda mazingira latamatika Paris AFP - EMMANUEL DUNAND
Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo mwenyeji wa mkutano huu nchi ya Ufaransa, ikisema kongamano hili ni kwaajili ya zoezi la kutafuta muafaka wa pamoja, viongozi wako kwenye shinikizo kuhakikisha wanatoa kauli thabiti kuhusu namna ya kutatua mkwamo wa kiuchumi uliotokana na msururu wa madeni kwa nchi masikini.

Mkutano huu unafanyika wakati ambapo kumekuwa na shinikizo kuhusu kubadili mfumo wa kidunia wa kifedha, ambao baadhi ya nchi zimesema umekuwa ukizinufaisha nchi tajiri ambazo zina maslahi.

Hata hivyo licha ya viongozi wengi kuzungumza lugha moja kuhusu namna bora ya kupata fedha kuzisaidia nchi zinazoendelea kukabiliana na madhara ya tabianchi, bado viongozi wanatofautiana pakubwa kuhusu mfumo utakaotumika kupata fedha hizo.

Nchi ya Barbados imeweka mezani mpango mkakati wa kutatua changamoto za kifedha kwa nchi zinazoendelea, mpango ambao umeungwa mkono huku shirika la fedha duniani IMF likiahidi kutoa dola bilioni 100.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.