Pata taarifa kuu

WHO Kutumia mfumo wa digitali kupambana na majanga

NAIROBI – Shirika la afya duniani, WHO, limesema litatumia cheti cha kidijiti kinachotumiwa na nchi za umoja wa Ulaya kama msingi wa kuwa na mfumo wa pamoja wa utoaji hati kuonesha mtu amechanjwa.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Katibu mkuu wa WHO
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Katibu mkuu wa WHO AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake WHO imesema janga la Uviko19 lilionesha umuhimu wa kuwa na mfumo wa pamoja wa kidijiti katika kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.

Mkurugenzi wa shirika hilo Tedros Adhanom Ghebreyesus, akizungumza baada ya kutiliana saini mkataba wa ushirikiano na umoja wa Ulaya, amesema majanga ya kiafya yaliyoshuhudiwa hivi karibuni, yamedhihirisha ni kwanini dunia inahitaji kuwa na mfumo kama huu.

Tedros ameongeza kuwa, mfumo huu unalenga kusaidia watu kutosumbuliwa wanapotoka nchi moja kwenda nyingine kwakuwa watakuta taarifa zao katika nchi wanaokoingia na kwamba utarahisisha upatikanaji wa takwimu za afya kwa wakati.

Kwa upande wake EU, inasema mfumo huu wa kidijiti utahuisha huduma zote za afya zinazohusiana na chanjo na kwamba itakuwa rahisi kwa wasafiri na raia wengine kupata huduma haraka.

Wakati wa janga la Uviko 19, EU ilizindua mfumo wa kidijiti ambao uliwalazimisha raia wake kuwa na cheti cha mtandao kumuwezesha kusafiri licha ya kuwa mfumo wa kawaida pia unatumika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.