Pata taarifa kuu

Hali ya wasiwasi yaongezeka kaskazini mwa Kosovo

NAIROBI – Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amesema maofisa wa Serikali ya Kosovo wanawajibika kutokana na vurugu zilizoshuhudiwa wiki hii wakati wa uchaguzi wa Serikali za mitaa ambapo watu zaidi ya 80 walijeruhiwa.

Maofisa wa usalama wametumwa katika maeneo hayo kuzuia machafuko
Maofisa wa usalama wametumwa katika maeneo hayo kuzuia machafuko © Dejan Simicevic / AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa sasa hali ni ya utulivu licha ya uwepo wa hofu ya kutokea makabiliano mengine kati ya jamii za Wakosovo na Waserbuia wanaoishi Kosovo.

Macron, amesema ni wazi machafuko yaliyoshuhudiwa juma hili yalichochewa na viongozi wa Kosovo, ambao walikadi makubaliano yaliyopo kuhusu jamii ya Waserbia wanaishi kwenye nchi hiyo.

Kauli ya Macron, ni kama ile ya rais wa Urusi, Vladmir Putin, ambaye kupitia kwa msemaji wake Dmitry Peskov, amesema haki za Waserbia waishio Kosovo lazima ziheshimiwe.

Tayari Jumuiya ya NATO imetuma wanajeshi wake wa kulinda amani kwenye eneo la Mpaka wa Kosovo.

Vurugu za juma hili zilizuka baada ya raia wakiserbia kujaribu kuingia katika ukumbi wa manispaa kupiga kura, lakini hata hivyo baada ya kukataliwa walifanya vurugu.

Mwanzoni mwa mwezi huu, waziri mkuu wa Kosovo, Albin Kurti na rais wa Serbia Aleksandar Vucic, walikutana Brussels Ubelgiji kujaribu kumaliza mzozo uliopo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.