Pata taarifa kuu

Tedros: Ugonjwa wa Mpox sio janga tena ulimwenguni

NAIROBI – Shirika la afya duniani WHO, limetangaza kuwa ugonjwa wa MPox sio janga tena ulimwenguni.

Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO)
Tedros Adhanom Ghebreyesus, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hili linakuja mwaka mmoja baada ya ugonjwa huo uliokuwa ukijulikana kama MonkeyPox kuanza kusambaa kote ulimwenguni.

Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, amesema uamuzi huo umechangiwa na kushuka kwa matukio ya ugonjwa huo, lakini amesisitiza kuwa ugonjwa huo bado ni tishio, hasa katika maeneo ya Afrika ambako umekuwepo kwa muda mrefu.

Ni wiki moja sasa tangu shirika hilo kutangaza kuwa Uviko 19, sio janga tena.

Licha ya kuwa kwa muda mrefu katika sehemu za Afrika ya Kati na Magharibi, mnamo mwezi Mei mwaka jana visa vya ugonjwa huo vilianza kuibuka Ulaya, Amerika Kaskazini kisha kwingineko, hasa miongoni mwa wanaume wanaoshiriki ngono na wanaume wengine.

Zaidi ya matukio 87,000 na vifo 140 vimeripotiwa kutoka nchi 111 wakati wa mlipuko wa kimataifa, kulingana na rekodi ya WHO.

Kulingana na Tedros, takriban asilimia 90 ya kesi chache zilirekodiwa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, ikilinganishwa na kipindi cha miezi mitatu ya hapo awali.

Virusi vya monkeypox ambavyo husababisha ugonjwa wa mpox huambukizwa kwa mtu kugusana na mwingine, au wanyama walioambukizwa.

Ugonjwa huu uligunduliwa kwa mara ya kwanza kwa wanadamu mnamo 1970 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.