Pata taarifa kuu

Papa Francis anawataka raia wa Hungary 'kufungua milango' kwa wahamiaji

Nairobi – Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amewataka raia wa Hungary kufungua milango kwa wahamiaji, huku akimaliza ziara yake ya siku tatu nchini humo, taifa ambalo linaongozwa na baraza la mawaziri la kitaifa linalopinga uhamiaji.

Papa Francis akihutubia wahumini jijini Vatican - Machi, 29 ,2023.
Papa Francis akihutubia wahumini jijini Vatican - Machi, 29 ,2023. © via REUTERS - VATICAN MEDIA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika misa katika mji mkuu wa Budapest, Papa Francis alisema kuwa inasikitisha na ni uchungu kuona milango ikifungwa kwa watu.

Takriban waumini 100,000 walihudhuria misa hiyo, akiwemo Waziri Mkuu wa Hungary Viktor Orban.

Bw Orban amekuwa mkosaji mkubwa wa uhamaji, huku akilazimika kujenga ua wa mpakani ili kuwazuia wahamiaji kuvuka kuingia Hungary.

Akihutubia umati karibu na jengo la bunge la Hungary siku ya Jumapili, Papa Francis aliomba kila mtu ikiwa ni pamoja na wale walio na majukumu ya kisiasa na kijamii kuwa wazi zaidi.

Wakati wa misa hiyo, papa wa Argentina, pia alirejelea uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine ulioanzishwa mnamo Februari 2022.

Aliwaombea raia wa ukraine waliokuwa wamekata tamaa na vile vile raia wa Urusi kwamba wawe na matumani kwamba amani itapatikana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.