Pata taarifa kuu

Yemen: Watu 78 wamethibitishwa kufariki katika mkanyagano

NAIROBI – Watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa hafla ya kusambaza  misaada kwa ajili ya ramadhani, maofisa katika eneo hilo wamethibitisha.

Watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa hafla ya kusambaza  misaada kwa ajili ya Ramadhani.
Watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa hafla ya kusambaza misaada kwa ajili ya Ramadhani. AP
Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo limetokea  katika Jiji la Kale katikati mwa mji wa Sanaa wakati mamia ya watu masikini walipokusanyika katika hafla iliyoandaliwa na wafanyabiashara kwa ajili ya kutoa msaada.

Kwa mujibu wa mseaji wa wazara ya mambo ya ndani, tukio hilo lilisababishwa na ukosefu wa uratibu mwafaka kutoka kwa mamlaka za mitaa wakati wa kugawa nasimu za fedha .Majeruhi walipelekwa katika hospitali za karibu kupata huduma za matibabu.

Kanda za video kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha matukio ya fujo baada ya tukio hilo katika eneo la Bab-al-Yemen mjini humo. Mamia ya watu walimiminika katika shule hiyo kupokea michango ambayo ilikuwa takriban $9 (£7) kwa kila mtu.

Picha zilizochukuliwa kutoka kwa video zikionyesha hali ilivyokuwa baada ya tukio la mkanyagano nchini Yemen
Picha zilizochukuliwa kutoka kwa video zikionyesha hali ilivyokuwa baada ya tukio la mkanyagano nchini Yemen AP

Waasi wa Houthi wamekuwa wakitawala mji huo tangu walipoiondoa serikali mwaka wa 2015.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani, waliohusika na usambazaji huo wamezuiliwa na uchunguzi unaendelea wakati waandaaji wa mpango huo wakituhumiwa kwa kukosa kufuata utaratibu wa kutoa fedha bila kuwashusisha viongozi wa eneo hilo.

Aidha imeripotiwa kuwa idadi kubwa ya raia walijeruhiwa , kumi na tatu kati yao wakiwa katika hali mbaya.

Watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa hafla ya kusambaza  misaada kwa ajili ya Ramadhani, maofisa katika eneo hilo wamethibitisha.
Watu 78 wameuawa katika mkanyagano katika shule moja kwenye mji mkuu wa Yemen Sanaa wakati wa hafla ya kusambaza misaada kwa ajili ya Ramadhani, maofisa katika eneo hilo wamethibitisha. AP

Tukio hilo lilitokea wakati wa siku za mwisho za mwezi mtukufu wa Waislamu wa Ramadhani, ambao huadhimishwa na kipindi cha mfungo.

Yemen imeathirika na mzozo ulioongezeka tangu mwaka wa 2015, wakati ambapo wapiganaji wa Houthi walipochukua udhibiti wa maeneo makubwa ya magharibi mwa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.