Pata taarifa kuu

Ukuaji wa uchumi unadorora barani Afrika, yaonya IMF

Ripoti ya Shirika la Fedha la Kimataifa, IMF, inaeleza kuwa Waafrika milioni 132 walikabiliwa na hali mbaya ya ukosefu wa chakula mwaka jana na kwamba uchumi wa Kusini mwa Jangwa la Sahara utashuka kwa asilimia 3.6 mwaka huu kulingana na Luc Eyraud, mkurugenzi wa masuala ya utafiti na tathmini ya kikanda katika IMF.

Ukuaji wa uchumi ulionekana kustahimili kwa kushangaza katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2022, kulingana na IMF.
Ukuaji wa uchumi ulionekana kustahimili kwa kushangaza katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2022, kulingana na IMF. Getty Images - John Seaton Callahan
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), uchumi wa dunia unatarajiwa kudorora mwaka huu 2023 kabla ya kuongezeka tena mwaka 2024, likitaja sababu za kufunguliwa tena kwa ghafla kwa China baada ya kumalizika kwa sera yake ya "sifuri Uviko-19", na hali ya baridi kal , huko Ulaya. IMF inakadiria kuwa ukuaji utakuwa 2.9% mwaka huu na utafikia 3.1% mnamo 2024.

"Ukuaji utasalia kuwa dhaifu kwa viwango vya kihistoria, wakati mapambano dhidi ya mfumuko wa bei na vita vya Ukraine vinazikabili shughuli mbalimbali," amesema Pierre-Olivier Gourinchas, mwanauchumi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa, katika makadirio yaliyochapishwa Jumatatu Januari 30. Anaendelea kuwa mtazamo huu "unaweza kuwakilisha hatua ya kugeuka, na kushuka kwa ukuaji na kushuka kwa mfumuko wa bei".

Ukuaji wa uchumi ulionekana kustahimili kwa kushangaza katika kipindi cha miezi mitatu ya mwisho ya mwaka 2022, kulingana na IMF. "Mfumuko wa bei pia unatarajiwa kuimarika, ingawa mfumko mkuu wa bei, ambao haujumuishi bei tete ya nishati na vyakula, bado haujafikia kilele katika zaidi ya 80% ya nchi," amesema.

Kulingana na IMF, mambo haya, pamoja na kudhoofika kwa dola ya Marekani kutoka kilele chake mwezi Novemba, yameleta afueni kwa nchi zinazoinukia na zinazoendelea. Pia inaonyesha kuwa kushuka kutaonekana zaidi kwa wenzao matajiri. "Kupungua kwa kasi kunapaswa kuzingatiwa katika nchi tisa kati ya kumi zilizoendelea. Wanapaswa kuona ukuaji wao ukiongezeka kutoka 2.7% mwaka jana hadi 1.2% mwaka huu, kisha hadi 1.4% mnamo 2024", anaendelea Pierre-Olivier Gourinchas, mwanauchumi mkuu wa Shirika la Fedha la Kimataifa.14. Mashtaka mawili yalisomwa dhidi yake. Anakabiliwa na kifungo cha miaka mingi jela.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.