Pata taarifa kuu

Nchi maskini zaghadhabishwa na mataifa tajiri

NAIROBI – Viongozi kutoka nchi masikini duniani, mwishoni mwa juma lililopita, walionesha kukasirishwa na kutoridhishwa na namna nchi tajiri zimeendelea kunufaika na hali duni kwenye nchi zao, kitendo walichosema hakikubaliki.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Antonio Guterres akihutubu katika mkutano wa nchi maskini duniani jijini Doha Machi, 4, 2023.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Antonio Guterres akihutubu katika mkutano wa nchi maskini duniani jijini Doha Machi, 4, 2023. AFP - KARIM JAAFAR
Matangazo ya kibiashara

Wakizungumza katika kongamano linalofanyika Doha, Qatar, viongozi hao hawakuficha kile walichosema ubinafsi wan chi tajiri katika kutumiza ahadi za misaada kwa mataifa hayo.

Ni kauli ambayo ilipazwa na katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres.

“Maendeleo ya kiuchumi bado ni changamoto wakati huu nchi zikikabiliwa na njaa, zikizama katika madeni na kuendelea kutaabika kutokana kutokuwepo kwa usawa uliosababishwa na uviko 19.”ameeleza Antonio Guterres.

Guteress, ameyalaani mataifa ya tajiri duniani na kampuni za nishati kwa kuendelea kuyatoza mataifa masikini kiasi kikubwa cha faida, wanapoipa mikopo wakati huu bei ya nishati inapoendelea kupanda.

Akizungumza nchini Qatar kwenye kongamano la mataifa yanayokua, Guteress ameyataka mataifa hayo tajiri kutoa Dola Bilioni 500 kila mwaka kuyasaidia mataifa masikini.

Rais wa Burundi Évariste Ndayishimiye na mwenzake wa Malawi Lazarus Chakwera ni miongoni mwa waliohudhuria mkutano huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.