Pata taarifa kuu

Nchi maskini zaidi kufanya mkutano wa kilele mjini Doha ili kupata usikivu wa dunia

Viongozi wa nchi zenye maendeleo duni (LDCs) watatoa maombi mapya ya usaidizi katika mkutano wa kilele utakaofunguliwa mjini Doha siku ya Jumapili, wakitarajia kuvuta hisia za ulimwengu katika wakati mgumu.

Mji mkuu wa Qatar, Doha.
Mji mkuu wa Qatar, Doha. AP - Saurabh Das
Matangazo ya kibiashara

Madhara ya janga la Corona, athari za vita vya Ukraine kwenye usambazaji wa chakula na mafuta na vita vya gharama kubwa dhidi ya mabadiliko ya Tabia nchi ni mbaya kwa nchi tajiri, lakini mbaya zaidi kwa watu bilioni 1.3, sawa na 14% ya watu wanaoishi duniani wanaoishi katika nchi 46 zenye maendeleo duni (LDCs).

"Migogoro mingi inayoendelea leo ni mbaya zaidi katika nchi zenye maendeleo duni (LDCs)," amesema Agnes Chimbiri-Molande, Balozi wa Malawi katika Umoja wa Mataifa na Msemaji wa LDCs katika UN.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na viongozi na wawakilishi kutoka nchi 33 za Afrika, nchi 12 za Asia-Pacific na Haiti watakutana miongo mitano baada ya Umoja wa Mataifa kuunda kundi la LDC kwa madhumuni ya kutoa msaada maalum wa kimataifa kwa wanachama walio hatarini zaidi na wasio na uwezo.

Mpango wa utekelezaji kwa nchi hizi ulipitishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka jana. Walakini, hakuna ahadi ya mchango mkubwa wa kifedha inayotarajiwa katika mkutano wa kilele wa Doha, ambao umeahirishwa mara mbili kwa sababu ya UVIKO. Maelfu ya wataalam na wanaharakati pia wanatarajiwa nchini Qatar ambapo LDCs wanataka kuhakikisha kuwa ahadi zinatekelezwa na kutoa msukumo mpya, kulingana na wataalam.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.