Pata taarifa kuu

UN yaonya kuhusu kuendelea kuzorota kwa haki za binadamu duniani

NAIROBI – Katibu mkuu wa umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, ameonya kuhusu kuendelea kuzorota kwa ulinzi wa haki za binadamu duniani, akitolea mfano vurugu zinazoshuhudiwa kwenye maeneo mbalimbali kuanzia Ukraine, Ethiopia, DRC na Afrika Magharibi.

Mkutano kuhusu haki za binadamu mjini Geneva
Mkutano kuhusu haki za binadamu mjini Geneva REUTERS - DENIS BALIBOUSE
Matangazo ya kibiashara

Akihutubia mkutano wa baraza la tume ya haki za binadamu ya umoja wa Mataifa, Guterres, amesema hali huenda ikawa mbaya zaidi, ikiwa nchi zitaendelea kupuuza ulinzi wa haki za msingi za binadamu.

“Kila siku tunapata ushahidi mpya wa ukiukaji wa haki za binadamu kuaanzia mauaji, mateso, kupotezwa na ukatili wa kigono.”ameeleza Antonio Guterres.

Serikali za mataifa ya bara Afrika zimekuwa zikitakiwa kuwaadhibisha wahusika wa vitendo vya ukiukaji wa haki za binadamu,baadhi ya viongozi wakituhumiwa kwa kuchangia katika ukiukaji wa haki za binadamu kwa kuminya uhuru wapinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.