Pata taarifa kuu
WHO - AFYA

WHO yatoa wito wa kuchangiwa dola za Marekani bilioni 2.4

Shirika la afya duniani, limetoa mwito wa kuchangiwa kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.4 kwa mwaka 2023 ili kusaidia mamilioni ya raia duniani ambao wanakabiliwa na majanga ya dharura ya kiafya. 

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus
Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus AP - Salvatore Di Nolfi
Matangazo ya kibiashara

Mkurugenzi wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus, anasema kwa sasa wanakabiliana na idadi kubwa ya majanga ya kiafya kwenye nchi za Pembe ya Afrika, ukanda wa Sahel na eneo la mashariki ya kati. 

“Tunapouanza mwaka wa 2023, tunashuhudia muunganiko wa majanga ambayo yanahitaji hatua za madhubuti kuchukuliwa.”ameeleza Tedros Adhanom Ghebreyesus

Majanga kama vile uviko 19, mlipuko wa Ebola na kipindupindu katika baadhi ya mataifa duniani, yakitajwa kuwa mojawapo ya majanaga yanayowatatiza raia duniani. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.