Pata taarifa kuu
UCHUMI- DUNIA

IMF: Mwaka wa 2023 utakuwa na changamoto zaidi ya 2022

Uchumi wa mataifa mengi duniani, unatarajiwa kuendelea kukua kwa kasi ndogo huku hali ikibashiriwa kuwa ngumu zaidi mwaka huu 2023, kutokana na uchumi wa mataifa mengi yenye nguvu kudorora ikiwemo China na Marekani.

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani, IMF, Kristalina Georgieva
Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani, IMF, Kristalina Georgieva REUTERS - MICHELE TANTUSSI
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mkurugenzi wa shirika la fedha duniani, IMF, Kristalina Georgieva, Uchumi wa China utakua kwa kasi ndogo kutokana na masharti ya Uviko19 na kusababisha athari kwa dunia.

“Katika kutoa chanjo imekuwa nyuma, haijafanya kazi vizuri namna bora ya kupata chanjo na kuitoa kwa wanachi.” amesmea Kristalina Georgieva.

Hali kama hii itashuhudiwa barani Ulaya na Marekani, licha ya kuwa huenda zisitumbukie katika mzozo wa kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.