Pata taarifa kuu
SIKUKUU YA KRISMASI

Wakiristo waadhimisha sikukuu ya Krismasi kote duniani

Wakiristo kote duniani, leo wanaadhimisha sikukuu ya Krismasi au Noeli, siku muhimu katika kalenda ya imani yao. 

Maadhimisho ya Krismasi mwaka 2021
Maadhimisho ya Krismasi mwaka 2021 REUTERS/Mussa Qawasma
Matangazo ya kibiashara

Sikukuu ya Krismasi ni siku ambayo Wakiristo wanasherehekea kuzaliwa kwa Yesu Kristo, mwokozi wao, wanayeamini alizaliwa zaidi ya miaka Elfu iliyopita, ili kuja kuwakomboa katika ulimwengu huu. 

Waumini hao wanakusanyika Makanisani na maeneo mengine ya kuabudu kuanza maadhimisho haya, huku wengine wakitumia siku hii, kutalii katika maeneo mbalimbali. 

Kwa mara ya Kwanza, baada ya miaka miwili, sikukuu ya Krismasi inaseherehekewa bila ya vikwazo vya maambukizi ya Uviko 19 baada ya kushuka kwa kiwango cha maambukizo. 

Mjini Bethlem, nchini Israeli alikozaliwa Yesu Kristo, maelfu ya mahujaji wanaadhimisha siku hii muhimu ambayo inafanyika wakati dunia ikabiliwa na changamoto mbalimbali, vita kati ya Urusi na Ukraine, mamilioni ya watu hasa  nchi za êneo la  pembe ya Afrika wakikabiliwa na baa la njaa, lakini pia baadhi ya mataifa yakikabiliwa na utovu wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.