Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA 2022

Argentina ndio mabingwa wa kombe la dunia, waishinda Ufaransa

Argentina imeshinda kombe la dunia katika mchezo wa soka,  baada ya kuwafunga waliokuwa mabingwa, Ufaransa kwa mabao 4 kwa 2 kupitia mikwajo ya penalti, katika fainali ya kuvutia, iliyopigwa Jumapili, Desemba 18 nchini Qatar.

 Lionel Messi, akiongoza wachezaji wenzake kusherehekea kombe la dunia, baada ya kuishinda Ufaransa, mabao 4-2, Desemba 18 2022, kupitia mikwaju ya penalti
Lionel Messi, akiongoza wachezaji wenzake kusherehekea kombe la dunia, baada ya kuishinda Ufaransa, mabao 4-2, Desemba 18 2022, kupitia mikwaju ya penalti AP - Martin Meissner
Matangazo ya kibiashara

Hili ni taji la tatu kwa nchi ya Argentina katika historia yake ya kombe la dunia, baada ya kushinda taji lake la pili mwaka 1986.

Katika kipindi cha pili cha fainali hiyo, inayoelezwa kuwa ya kipekee, Ufaransa iliyokuwa imefungwa mabao 2 kwa 0 kipindi cha kwanza, ilitoka nyuma na kusawazisha mabao yote mawili, kupitia nyota wake, Kylian Mpappe.

Mechi hiyo ilikwenda katika muda wa ziada, na kuishia sare ya mabao 3 kwa 3, na ikabidi bingwa apatikane kwa mikwaju ya penalti.

Sherehe zimeendelea katika jiji kuu la Argentina, Buenos Aires, raia wa nchi hiyo, wakimsifia Messi kwa kusaidia nchi yao kuibuka mshindi.

 

Mashabiki wa Argentina
Mashabiki wa Argentina REUTERS - AGUSTIN MARCARIAN

“ Siamini, nimekuwa nikilia tu, nilitamani sana kumwona Messi, nilipomwana machozi yakanizidi. Nimefurahi sana, siku zote nimekuwa na imani kwa sababu ya Messi, hakika alistahili kushindi kwa sababu huenda hii ni mara ya mwisho kuichezea timu ya taifa ,” amesema Lucila

Huu sio ushindi wa Messi tu, tulistahili kushinda wote, tumepitia magumu kama nchi, lakini ushindi huu, umetupa furaha kubwa. Tunasherehekea tu," Amesema shabiki mwingine Benjamin.

Nahodha wa Argentina Lionell Messi, amesema  hatimaye haya ya moyo wake imetimia baada ya kushinda taji hilo la kombe la dunia.

Lionell Messi naye pia amehusishwa na kuhamia nchini Saudi Arabia akitokea nchini Ufaransa
Lionell Messi naye pia amehusishwa na kuhamia nchini Saudi Arabia akitokea nchini Ufaransa AP - Martin Meissner

“Namshukuru sana Mwenyezi Mungu, amenijalia mengi, hakika kiu yangu imekuwa ni kushinda taji hili,” Messi amesema.

Kuelekea katika fainali hii, Messi mwenye umri wa miaka 35, alikuwa amedokeza kuwa, itakuwa fainali yake ya mwisho, kuichezea timu ya taifa.

 Wakati, Ufaransa wakihuzunishwa na matokeo hayo, wafuasi wa Argentina duniani, wameendelea kusherehekea ushindi huu muhimu katika historia ya mchezo wa soka duniani, wakisubiri fainali nyingine mwaka 2026.

Mengine:

Taji la mchezajo bora katika mashindano haya, lilimwendea, Lionell Messi.

Kylian Mbappé mfungaji bora wa mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar
Kylian Mbappé mfungaji bora wa mashindano ya kombe la dunia nchini Qatar REUTERS - KAI PFAFFENBACH

Kylian Mbappe, alipata tuzo ya mfungaji bora, kwa kufuga mabao 8 katika mashindano haya.

Emiliano Martinez raia wa Argentina, alishinda taji la kipa bora.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.