Pata taarifa kuu

OECD: Ukuaji wa kimataifa utashuka hadi 2.2% mnamo 2023

Ongezeko la bei linatarajiwa kuwa wastani wa 8% mwaka huu katika nchi za G20 kulingana na shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OECD.

Bandari ya Los Angeles, California.
Bandari ya Los Angeles, California. © AP Photo/Damian Dovarganes)
Matangazo ya kibiashara

Ukuaji wa uchumi wa dunia utapiga hatua, kutoka 3.1% mwaka 2022 hadi 2.2% mwaka ujao, kabla ya kuongezeka tena hadi 2.7% mwaka 2024, kulingana na utabiri wa hivi karibuni kutoka shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo, OECD, uliyochapishwa leo Jumanne.

Kutokana na hali ya vita nchini Ukraine, "ukuaji uko nusu mlingoti, mfumuko wa bei unaendelea, imani imepungua na kutokuwa na hofu imezidi kupanda," labainisha shirika la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo.

"Uchumi wa kimataifa unakumbwa na mzozo mbaya zaidi wa nishati tangu miaka ya 1970," amesema kaimu mchumi mkuu wa OECD, Alvaro Santos Pereira.

"Mshtuko wa nishati umeleta mfumuko wa bei kwa viwango ambavyo havijaonekana katika miongo kadhaa na kupunguza ukuaji kila mahali ulimwenguni", ameongeza mwanauchumi.

Kupanda kwa bei kunapaswa kufikia 8% kwa wastani mwaka huu katika nchi za G20, ambayo ni pamoja na chumi kuu ulimwenguni, kabla ya kushuka hadi 5.5% mnamo 2023 na 2024, kulingana na makadirio ya shirika hilo.

Bw Santos Pereira anaeleza kuwa hali inayowezekana zaidi inayotarajiwa na OECD "siyo mdororo wa kiuchumi duniani, lakini kushuka kwa kasi kwa uchumi wa dunia mwaka 2023, pamoja na mfumuko wa bei ambao bado uko juu, lakini unapungua katika nchi nyingi".

Ili kuondokana na mzozo huo, OECD, shiŕika ambalo linaleta pamoja Mataifa 38, nchi zilizoendelea na nchi chache zinazoinukia, linatetea “kuendelea kukaza sera ya fedha ili kukabiliana na mfumuko wa bei” huku ikizingatiwa kwamba “msaada wa kibajeti unapaswa kulengwa zaidi na wa muda mfupi”.

"Kuongeza kasi ya uwekezaji ili kupitisha na kuendeleza vyanzo na teknolojia ya nishati safi itakuwa muhimu kwa uchanganuzi na kuhakikisha usalama wa nishati," mwanauchumi huyo amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.