Pata taarifa kuu

Guterres: Viongozi wanatakiwa kuikumbatia dunia

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito wa ushirikiano wa kidunia, kutatua changamoto zinazoikabili dunia kama umasikini,  baa la njaa na mabadiliko ya tabia nchi. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema iwe ni Pakistan, Pembe ya Afrika au Sahel, nchi za visiwa vidogo au zinazoendelea, suala ni kwamba nchi zilizo hatarini zaidi ambazo hazijasababisha janga la tabianchi ndio zinaathirika na janga lililochochewa na wachafuzi wakuu wambao ni kutoka nchi za kundi la nchi 20 au G20.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema iwe ni Pakistan, Pembe ya Afrika au Sahel, nchi za visiwa vidogo au zinazoendelea, suala ni kwamba nchi zilizo hatarini zaidi ambazo hazijasababisha janga la tabianchi ndio zinaathirika na janga lililochochewa na wachafuzi wakuu wambao ni kutoka nchi za kundi la nchi 20 au G20. © REUTERS / Jeon Heon-Kyun
Matangazo ya kibiashara

Katika kuelekea mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa unaoanza wiki ijayo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres amesema ujumbe wake mkuu kwa viongozi watakaoshiriki mkutano huo ni dhahiri ya kwamba wachukue hatua kupunguza kiwango cha joto duniani

Guteress ametoa wito huu wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 77 wa Umoja wa Mataifa jijini New York. 

Ametaja tishio hilo kuwa ni pamoja na mgawanyiko mkubwa wa kijiografia na kimkakati, mgawanyiko aliosema ni mkubwa kuwahi kutokea tangu zama za vita baridi.

"Mgawanyiko huu unakwamisha hatua za pamoja za kukabiliana na changamoto zinazotukabili. Dunia imekumbwa na vita, changamoto za tabianchi, chuki zimezaga, na aibu kubwa inakabili dunia kutokana na umaskini, njaa na ukosefu wa usawa," amesema Guterres.

Akifafanua kuhusu tabianchi amerejelea kile alichoshuhudia wakati wa ziara yake ya kuonesha mshikamano na Pakistani ambayo imekumbwa na mafuriko makubwa.

Wiki ijayo, mkutano huo utahudhuriwa na wakuu wa nchi mbalimbali za dunia, kujadiliana kuhusua masuala mbalimbali yanayoikumba dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.