Pata taarifa kuu

Mexico, Canada na Marekani zatakiwa kujiandaa kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino, ameyataka mataifa ya Mexico, Canada na Marekani kujiandaa vema kwa michuano ya kombe la dunia mwaka 2026 kwa kile alichokisema, inatarajiwa kuwa na mashabiki wengi.

Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino:
Rais wa Shirikisho la soka duniani FIFA, Gianni Infantino: REUTERS - KAI PFAFFENBACH
Matangazo ya kibiashara

Kwa mara ya kwanza, michuano ya kombe la dunia itahusihsa timu 48 kutoka 32 na eneo la Amerika Kaskazini litaandaa michuano hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994. 

Nchini Marekani , viwanja vinavyotumiwa kuandaa michuano ya soka la Marekani itaanda michuano hiyo huku uwanja wa MetLife ulio na uwezo wa kuwaingiza mashabiki Elfu 82  ulio katika jijini la New York ukitarajiwa kuandaa fainali. 

Nchini Mexico, uwanja wa Azteca utatumiwa na viwanja vingine vitatu katika miji ya Monterrey na Guadalajara, huku miji ya Vancouver na Toronto ikichaguliwa kuandaa mecjhi zitakazochezwa nchini Canada.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.