Pata taarifa kuu

Siku ya wanawake duniani yaadhimishwa

Nchi mbalimbali duniani zinaadhimisha Jumanne hii Machi 8 siku ya wanawake. Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa tarehe 8 Machi ya kila mwaka. Siku hiyo ilianza kuadhimishwa tarehe 8 Machi 1975 baada ya Umoja wa Mataifa kuridhia siku hii kutumika kama siku rasmi ya kuikumbusha dunia juu ya haki za wanawake.Siku hii pia huongeza chachu katika harakati za mapambano katika usawa wa kijinsia kwa wanawake na wanaume katika jamii.

Flopy Mendosa, Chantal Djédjé na Lérie Sankofa kutoka Abidjan kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
Flopy Mendosa, Chantal Djédjé na Lérie Sankofa kutoka Abidjan kwa ajili ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake. © Guillaume Ploquin / Photomontage RFI
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, siku ya Jumatatu, alisisitiza kwamba dunia haiwezi kujikwamua kutoka katika janga la COVID-19 kwa kurejesha saa nyuma katika suala la usawa wa kijinsia. 

Kupitia ujumbe wake wa siku hii Guterres ameainisha mchango mkubwa uliofanywa na wanawake katika jitihada za kutokomeza janga la COVID-19, na kupongeza mawazo yao, ubunifu wao na harakati zao ambazo zinaibadili dunia na kuifanya kuwa bora huku akikaribusha hatua ya kuwa na viongozi zaidi wanawake kote duniani katikia nyanja mbalimbali.

“mara kwa mara wanawake na wasichana wamebeba mzigo mkubwa wa athari za virusi vinavyosambaa duniani kote, ambazo ni pamoja na wasichana na wanawake kufungiwa shule na maeneo ya kazi, na kusababisha kuongezeka kwa umaskini na unyanyasaji, na kushuhudiwa kwa wanawake wengi kufanya idadi kubwa ya kazi zisizo na malipo duniani lakini za matunzo na huduma muhimu, ”  amesema Antonio Guterres.

Siku ya wanawake duniani kwa mara wa kwanza ilisherehekewa katika mwaka wa 1911 ambapo mataifa kumi na moja yalikusanya wanawake mia moja walipoanza kuadhimisha siku hii.

Mwaka 1908 jumla ya wanawake elfu kumi na tano waliandamana katika mji wa New York wakidai kupunguziwa muda wa kufanya kazi, kupata ujira wa kuridhisha na kupewa haki ya kupiga kura.

Mwaka 1909 mwanamke kwa jina la Clara Zetkin alipendekeza kuanzishwa kwa siku ya wanawake duniani katika mkutano wa wafanyakazi wanawake uliofanyika katika jiji la Copenhagen nchini Denmark.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.