Pata taarifa kuu
UFISADI-DEMOKRASIA

Ripoti: Ufisadi unazidi kushika kasi duniani, demokrasia inarudi nyuma

Mapambano dhidi ya rushwa yamedumaa katika muongo mmoja uliopita huku kukiwa na ongezeko la ukiukwaji wa haki za binadamu na kurudi nyuma kwa demokrasia, kulingana na ripoti ya hivi punde kutoka Shirika la kimataifa la kupambana na ufisadi la Transparency International.

Shirika la kimataifa la Transparency International inabainisha kuwa kuna uhusiano kati ya vita dhidi ya rushwa na demokrasia.
Shirika la kimataifa la Transparency International inabainisha kuwa kuna uhusiano kati ya vita dhidi ya rushwa na demokrasia. © Les Echos
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya mwaka 2021 inaonyesha kuwa katika 86% ya nchi 180 zilizofanyiwa uchunguzi, kumekuwa na uboreshaji mdogo au hakuna uboreshaji katika miaka kumi iliyopita. Shirika la kimataifa la Transparency International inabainisha kuwa kuna uhusiano kati ya vita dhidi ya rushwa na demokrasia.

"Tunaona tu uboreshaji mkubwa katika nchi 25 pekee duniani kote, [wakati] nchi 23 zimerudi nyuma," amesema Roberto Kukutschka, mratibu wa utafiti katika shirika la kimataifa la Transparency International.

Denmark, Finland na New Zealand ndio watendaji wazuri; zote zimepata alama 88 kati ya 100. Hakuna nchi ya Kiafrika iliyo kwenye orodha.

Hata hivyo maboresho makubwa yameonekana katika mataifa ya Baltic ya Estonia, Latvia, na Armenia.

"Hakuna uboreshaji mkubwa, hata hivyo,  Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini," kulingana na VOA ikimnukuu Kukutschka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.