Pata taarifa kuu
SIKUKUU YA MWAKA MPYA

Dunia yaukaribisha mwaka mpya wa 2022 licha ya kusambaa kwa Omicron

Dunia imeukaribisha mpya wa 2022 katika kipindi ambacho kirusi cha Omicron kinapoendelea kusambaa kwa kasi na kusababisha shamrashamra kusitishwa katika mataifa makubwa kama jijini Paris Ufaransa.

Heri ya mwaka mpya
Heri ya mwaka mpya Yuki IWAMURA AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika miji mbalimbali ya mataifa ya Ulaya na Marekani, kinyume na miaka iliyopita, watu walisalia majumbani, huku maeneo mengine kama New York, watu wachache wakiruhusiwa kuukaribisha mwaka mpya.

Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron katika hotuba yake ya mwisho wa mwaka 2021, ameonya kuwa maambukizi ya Covid 19 yakaongzeka mwezi huu, baada ya maambukizi makubwa ya zaidi ya Laki mbili kuripotiwa.

Barani Afrika, hali ilikuwa kama kwingineko duniani, huku wengi wakiamua kwenda katika majumba ya ibada huku viongozi wa mataifa mbalimbali wakitoa hotuba za mwisho wa mwaka.

Nchini Uganda, baada ya shule kufungwa kwa miaka miwili kutokana na janga la Covid 19, rais Yoweri Museveni, alitanagza kuwa Shule zitafunguliwa tena.

"Shule za msingi na sekondari, sitafunguliwa tena kuanzia Januari 10 naagiza Wiaza ya elimu na michezo kufanya kazi pamoja kuhusu taratibu na kuziweka wazi," amesema rais Museveni.

Nchini Tanzania rais Samia Suluhu Hassan, amesema miongoni mwa mambo ambayo serikali yake itafanya mwaka 2022 ni kupambana na ugonjwa corona.

Nchini Kenya, rais Uhuru Kenyatta amewaambia raia wa nchi yake, kufanya uchaguzi wa busara wakati wa uchaguzi Mkuu mwezi Agosti, kumchagua kiongozi imara.

"Lazima tuchague wale wachache,  wenye uthubutu kwa hivyo tunapoanza mwaka mpya, tukumbuke kuwa, kiongozi ni lazima  achukue njia ya uthubutu kwa ajili ya vizazi vijavyo, lakini mwanasiasa hukuchukua njia inayowafurahisha wengi, na hafiki  popote," amesema Kenyatta.

Rais wa DRC Felix Thisekedi katika ujumbe wake, amewataka vijana wa nchi hiyo kusaidia katika kuijenga taifa lao huku rais wa Rwanda Paul Kagame akitaka raia wa nchi yake kuendelea kuwa macho katika vita dhidi ya Covid 19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.