Chombo chenye nguvu chaondoka duniani kuzuru Orbit
Chombo chenye nguvu kimeondoka duniani kwenda kwenye njia ya Orbit nje ya dunia, umbali wa Kilomita Milioni 1. 5 kutoka duniani, baada ya majaribio ya siku kadhaa.
Imechapishwa:
Kituo cha James Webb Space Telescope, kimekuwa kikitumia Mabilioni ya Dola kufanikisha ujenzi wa chombo hicho kwa muda wa miongo mitatu, na kilirushwa kutoka eneo la Kourou huko French Guiana.
Inarajiwa kuwa, chombo hicho kinatarajiwa kufika katika njia hiyo ya Orbit na inatarajiwa kuwasaidia wanasayansi kuelewa kuhusu chimbuko la dunia.
Chombo hicho kilichoitwa kwa jina la Mkurugenzi wa NASA wa zamani , kinalenga pia kuonesha namna ulimwengu ulivyokuwa, karibu miaka Bilioni 14 iliyopita.