Pata taarifa kuu

COP26 : Zaidi ya nchi 80 zaahidi kupunguza uzalishaji wa Methane kwa 30% ifikapo 2030

Katika mkutano wa kujadili juu ya athari ya mabadiliko ya tabia nchi COP26 unaofanyika mjini Glasgow, nchini Scotland, zaidi ya nchi 80, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Ulaya na Marekani, zimeahidi kupunguza uzalishaji wa Methane kwa 30% ikilinganishwa na mwaka 2020 ifikapo 2030.

Kampuni ya uchimbaji wa methane katika maji ya Ziwa Kivu nchini Rwanda, Aprili 17, 2016.
Kampuni ya uchimbaji wa methane katika maji ya Ziwa Kivu nchini Rwanda, Aprili 17, 2016. PABLO PORCIUNCULA / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Methane (CH4) ni mojawapo ya gesi ambazo tunaweza kupunguza" na kupunguza "itapunguza mara moja ongezeko la joto duniani", ametangaza rais wa Tume ya Ulaya, Ursula von der Leyen, Jumanne hii katika mkutano wa COP26 huko Glasgow. Pia amekumbusha kuwa gesi hii inahusijka kwa "karibu 30%" ya ongezeko la joto duniani tangu Mapinduzi ya Viwanda.

Umoja wa Ulaya na Marekani wamekuwa wakifanya kazi juu ya makubaliano haya ya kupunguza uzalishaji wa Methane tangu katikati ya mwezi Septemba. Na tangu wakati huo, nchi nyingi zimejiunga na juhudi hizi kama vile Canada, Korea Kusini, Vietnam, Colombia na Argentina. Kwa jumla, nchi zilizotia saini ni 70% ya Pato la Taifa la kimataifa, Joe Biden amehakikisha.

Methane mojawapo ya gesi za Hydrocarbon ni gesi inayochangia katika ongezeko la joto duniani na huzalishwa katika usafirishaji na uzalishaji wa makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta. Mifugo, maeneo ya kutupa taka na tabia za kilimo pia huzalisha kiasi kikubwa cha gesi.

Methane mojawapo ya gesi za Hydrocarbon ni gesi inayochangia katika ongezeko la joto duniani na huzalishwa katika usafirishaji na uzalishaji wa makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta. Mifugo, maeneo ya kutupa taka na tabia za kilimo pia huzalisha kiasi kikubwa cha gesi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.