Pata taarifa kuu
UNSC-UCHAGUZI

Albania, Brazil, Gabon, Ghana na Falme za Kiarabu zachaguliwa UNSC

Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa leo Ijumaa umechagua Albania, Brazil, Gabon, Ghana na Falme za Kiarabu kama wanachama wapya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia Januari 1, 2022.

Ukumbi wa Mkutano Mkuu katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 18, 2015.
Ukumbi wa Mkutano Mkuu katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 18, 2015. REUTERS/Mike Segar
Matangazo ya kibiashara

Nchi hizo tano hazikukutana na upinzani wowote kwa kupitishwa kwenye baraza hilo lenye wanachama 15, wanaohusika na kuhakikisha amani na usalama wa kimataifa. Nchi hizozitachukua nafasi ya Estonia, Niger, Saint Vincent na Grenadines, Tunisia na Vietnam.

Ili kuhakikisha uwakilishi wa kijiografia, viti vinatengwa kwa makundi kulinana na kanda. Lakini hata kama nchi hizo hazikupata upinzani katika kundi lao, zitalazimika wkupata uungwaji mkono kwa zaidi ya theluthi mbili ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama ni chombo pekee cha Umoja wa Mataifa kinachoweza kuchukua maamuzi ya kisheria, kuanzia kuchukumliwa kwa vikwazo kwa idhini ya matumizi ya nguvu. Baraza hilo lina wanachama watano wa kudumu wenye nguvu ya kura ya turufu: Marekani, Uingereza, Ufaransa, Uchina na Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.